Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia umeongezeka asilimia 3.6% kutoka asilimia 3.3%.

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia  umeongezeka asilimia 3.6% kutoka asilimia 3.3%.

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia  Mwezi Juni ,2021 umeongezeka  hadi  asilimia 3.6% kutoka asilimia 3.3% kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2021. Akizungumza na waandishi wa Habari leo Julai 8,2021 jijini Dodoma Kaimu mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu[NBS] Bi.Ruth Minja amesema  kuongezeka kwa mfumuko 

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia  Mwezi Juni ,2021 umeongezeka  hadi  asilimia 3.6% kutoka asilimia 3.3% kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2021.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Julai 8,2021 jijini Dodoma Kaimu mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu[NBS] Bi.Ruth Minja amesema  kuongezeka kwa mfumuko  wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni,2021 kumechangiwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei za bidhaa zisizo za vyakula .

Kaimu mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi.Ruth Minja
Sauti ya Kaimu mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi.Ruth Minja

Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka mfumuko wa bei  ni pamoja na vitambaa  vya nguo kwa asilimia  8.5%,nguo za wanawake kwa asilimia 6.3%,viatu vya wanaume kwa asilimia 6.2%,kodi ya pango kwa asilimia 4.9%,vyakula kwenye migahawa kwa asilimia 5.6%,na gharama za malazi kwa asilimia 5.7%.

Bi.Minja amefafanua mfumuko wa bei wa bidhaa  za vinywaji baridi  kwa mwaka ulioishia  mwezi Juni ,2021  umepungua hadi asilimia   4.7%  kutoka asilimia 4.9% kwa mwaka ulioishia mwezi Mei,2021.

Aidha,Bi.Minja ameainisha mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo  ambapo nchini Kenya umeongezeka kwa asilimia 6.32%  kutoka asilimia 5.87%  huku nchini Uganda   ukiongezeka pia  hadi asilimia 2.0%  kutoka asilimia 1.9%.

Kwaupande wake Kaimu mkugenzi wa Takwimu  za Uchumi Daniel Masolwa amesema kuanzia mwezi huu ofisi hiyo itaongeza kuweka  takwimu za uzalishaji wa umeme,saruji,mwenendo wa utalii,idadi ya watumiaji wa simu hiyo ni  katika kurahisisha tathmini ya ufuatiliaji katika kutoa takwimu za muda mfupi  kupitia tovuti.

Kaimu mkugenzi wa Takwimu  za Uchumi Daniel Masolwa
Sauti ya Kaimu mkugenzi wa Takwimu  za Uchumi Daniel Masolwa

Na Barnabas kisengi Dodoma. Julai 08. 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »