Asilimia 50 ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI nchini yapo kwa kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35.

Dodoma  IMEELEZWA kuwa zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI nchini yapo kwa kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika Disemba mosi ya kila mwaka, Katibu Mkuu,Ofisi ya Waziri Mkuu

Dodoma 

IMEELEZWA kuwa zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI nchini yapo kwa kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika Disemba mosi ya kila mwaka, Katibu Mkuu,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Uwekezaji DOROTHY MWALUKO amesema umri huo ni kwa mujibu wa Sera ya vijana ya mwaka 2007.

Amesema hapa nchini hali ya maambukizi mapya bado ni tishio  hivyo kuna wajibu wakutekeleza mikakati yote ya kuhakikisha kunakuwa hakuna maambukizi mapya.

Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya siku hiyo MWALUKO amesema Kitaifa yatafanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwak ufanya shughuli mbalimbali na mgeni rasmi anatarajiwak uwa Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA.

Ametaja shughuli nyingine kuwa ni kuanzia novemba 25 hadi 29  ambapo kutakuwa na maonyesho maalum ya kundi la vijana na kutakuwa na kijiji cha vijana kitakachotoa huduma rafiki kwa vijana,novemba 26 na 27 kutakuwa na kongamano la kisayansi la kitaifa la kutathimini hali na mwlekeo wa udhibiti wa virusi vya Ukimwi na Ukimwi ikifuatiwa na mdahalo wa vijana Novemba 28 na mkutano wa kutathimini utekelezaji wa maazimio ya nchi za mashariki na kusini mwa bara la Africa.

Akitoa tathimini ya utekelezaji wa 90 tatu,Meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi kutoka wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dokta BEATRICE MUTAYOBA amesema hadi kufikia Juni mwaka huu kwenye 90 ya kwanza ya asilimia 83 ya watu wamepima na wanatambua hali zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa (TACAIDS)Dkt Leornad Maboko amesema katika kuhakikisha vijana wanakuwa na uelewa zaidi juu ya virusi hivyo wamekuwa wakitumia majukwaa mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu “Mshikamano wa Kimataifa tuwajibike kwa pamoja”.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »