JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia na Kenya.

Dodoma JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia wahamiaji haramu 12 ambao ni raia wa Nchini  Ethiopia Mmoja Kati yao anatokea Nchini Kenya. Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma,Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,Gilles Muroto amesema kuwa Raia hao wamekamatwa wiki iliyopita katika eneo la Wilaya ya  Kongwa ambapo walikuwa wakichenji Dolla. Kamanda Muroto

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto.

Dodoma 
JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia wahamiaji haramu 12 ambao ni raia wa Nchini  Ethiopia Mmoja Kati yao anatokea Nchini Kenya.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma,Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,Gilles Muroto amesema kuwa Raia hao wamekamatwa wiki iliyopita katika eneo la Wilaya ya  Kongwa ambapo walikuwa wakichenji Dolla.

Kamanda Muroto amesema kuwa Raia hao wenye asili ya Ethiopia walikuwa wamepakiwa kwenye Lori ambalo lilikuwa likiendeshwa na Dereva wa Kitanzania  likielekea Nchini jirani ya  Zambia ili kwenda Afrika ya Kusini.

Katika hatua nyingine,Kamanda Muroto amesema kuwa  hali ya usalama Mkoani  Dodoma imeendelea kuwa  shwari wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi kutokana na kutokuwepo kwa vitendo vya kihalifu.

Hata hivyo ametoa  wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma kutofumbia macho vitendo vyote vya kihalifu bali  wanapaswa kutoa taarifa kwa Jeshi hilo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »