Kuelekea siku ya kupinga ukatili wa kijinsia Novemba 25 hadi Disemba 10 , jamii imeshauriwa kupinga vitendo hivyo.

Dodoma. Katika kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Novemba 25 hadi Disemba 10 , jamii imeshauriwa kuungana kwa pamoja kupinga vitendo hivyo kwani vimekuwa na athari nyingi kwenye jamii ikiwemo kurudisha nyuma maendeleo ya mtu mmoja mmoja. Siku 16 za kupiga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ianyoongozwa na kituo cha kimataifa

Dodoma.

Katika kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Novemba 25 hadi Disemba 10 , jamii imeshauriwa kuungana kwa pamoja kupinga vitendo hivyo kwani vimekuwa na athari nyingi kwenye jamii ikiwemo kurudisha nyuma maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

Siku 16 za kupiga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ianyoongozwa na kituo cha kimataifa cha wanawake katika uongozi tangu maka 1991.

Chimbuko la siku 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia linatokana na mauji ya kinyama ya kina dada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominica mwaka 1990.

Akizungumza Ofisini kwake Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma Meneja utekelezaji wa miradi  ya Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (Children’s Dignity Forum CDF ) Bwana Evance Rwamuhuru amesema jamii inakila sababu ya kutoa taarifa juu ya vitendo hivyo.

Bwana Rwamuhuru ametoa wito kwa wanaume wanaopiga wenza wao kuachana na vitendo hivyo kwani vimekuwa vikiudhalilisha utu wa mwanamke.

Katika hatua nyingine amesema shirika lao limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuifikia jamii hasa kwenye utoaji wa Elimu ya kupinga vitendo vya ukatili ili jamii iweze kujua madhara ya vitendo hivyo.

Bwana Rwamuhuru ameeleza vitendo vya ukatili ambavyo hutokea zaidia wilayani mpwapwa ambavyo Ubakaji,mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi , ukatili  ambao umekuwa ukitokea ndani ya ndoa pamoja utelekezaji wa familia

Mwaka 1991 Umoja wa Mataifa Un ulichagua Novemba 25 iwe siku ya Kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia ambapo kilele chake huadhishimishwa Disemba 10 ya kila mwaka.

Maadhimisho ya maadhimisho ya mwaka  huu yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘’Tupinga Ukatili wa Kijinsia,Mabadiko yanaanza na Mimi’’

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »