Prof. Tumbo awataka wanaofanya tathimini ya uhakiki wa usalama wa chakula na lishe kufanya tathmini kwa kuzingatia mazingira husika.

Prof. Tumbo awataka  wanaofanya tathimini ya uhakiki wa usalama wa chakula na lishe  kufanya tathmini kwa kuzingatia mazingira husika.

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Profesa Siza Tumbo   imewataka wataalamu wanaofanya tathimini ya uhakika wa usalama wa chakula na lishe  kufanya tathmini hizo kwa kuzingatia mazingira husika kwa kuangalia mitazamo ya ndani ya nchi badala ya kutumia mifumo ya nje ambayo wakati mwingine hukosa uhalisia wa maisha ya watanzania. Profesa

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 


Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Profesa Siza Tumbo   imewataka wataalamu wanaofanya tathimini ya uhakika wa usalama wa chakula na lishe  kufanya tathmini hizo kwa kuzingatia mazingira husika kwa kuangalia mitazamo ya ndani ya nchi badala ya kutumia mifumo ya nje ambayo wakati mwingine hukosa uhalisia wa maisha ya watanzania.

Profesa tumbo amesema  hayo leo jijini dodoma wakati akizindua Mfumo wa Uchambuzi wa Uhakika wa Chakula na Lishe Tanzania (MUCHALI) unaoratibiwa na Shirika la kilimo na chakula  la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo.

Amesema hali ya kufanya tathmini nchini bado siyo sahihi kwani mara nyingi hutumika mbinu za Mataifa mengine katika kufanya tathmini za ndani ya nchi jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa marekebisho.

 Pia amewahimiza watanzania kuzingatia ulaji wa vyakula vya asili vinavyojenga kinga na kuimarisha afyua badala ya  kutumia vyakula vya kisasa ambavyo asilimia kubwa huchangia udhaifu wa kinga ya mwili kukabiliana na maradhi mbalimbali.

 Kwa upande wake  Mtaalamu wa  Lishe  kutoka Shirika la Mpango wa Kilimo na Chakula  la Umoja wa Mataifa (FAO),Stella Kimambo amesema muongozo uliozinduliwa utatathmini hali ya chakula na lishe kwa ngazi ya mkoa na wilaya na kuanisha  hatua muhimu ambazo zitakazochukuliwa na MUCHALI na wadau wengine wakati wa ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa taarifa za usalama wa chakula.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Uhakika wa Chakula na Lishe kutoka Zanzibar,Hamad Masoud Ali ameahidi kufanya mabadiliko ya muongozo wa tathmini ya usalama wa chakula na lishe kwa upande wa Zanzibar kufuatia mabadiliko ya kisera ikiwemo muundo wa serikali za mitaa ambao awali haukuwepo ili kufanikisha zoezi hilo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »