KUFUATIA UPUNGUFU WA MADARASA, WANAFUNZI ZAIDI YA 100 WASOMEA DARASA MOJA.

KUFUATIA UPUNGUFU WA MADARASA, WANAFUNZI ZAIDI YA 100 WASOMEA DARASA MOJA.

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Shule ya Msingi Michese iliyopo Kata ya Mkonze Jijini Dodoma inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya Madarasa hali inayopelekea wanafunzi zaidi ya mia moja kusomea katika chumba kimoja ambapo ni hatari sana ukizingatia kumekuwa na ugonjwa wa covid 19 na wanafunzi wengine kukaa chini kwa ukosefu wa madawati shuleni hapo licha shule

Na Barnabas Kisengi-Dodoma

Shule ya Msingi Michese iliyopo Kata ya Mkonze Jijini Dodoma inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya Madarasa hali inayopelekea wanafunzi zaidi ya mia moja kusomea katika chumba kimoja ambapo ni hatari sana ukizingatia kumekuwa na ugonjwa wa covid 19 na wanafunzi wengine kukaa chini kwa ukosefu wa madawati shuleni hapo licha shule hii kuwa katikati ya jiji la Dodoma.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Dodoma ANTONY MTAKA baada ya kufanya ziara katika shule hiyo ambapo alikuwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini. Mbunge wa Jimbo la Dodoma.

Kaimu mkurugenzi na watendaji wa idara ya elimu wa halmashauri ya jiji la Dodoma.

Awali akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya msingi Michese Mwalimu SIZYA WILLAM amesema shule hiyo inajumla ya wanafunzi 1850, vyumba vya madarasa tisa na inaupungufu wa madawati na haina vyoo vya walimu ambao kwa sasa wanajisaidia kwa kuchanganyika kwa kutumia vyoo vya wanafunzi na kwa majirani na shule hiyo.

“Hapa kwakwweli mkuu wa mkoa shule yetu inakabiliwa na changamoto nyingi kama ulivyo ona wanafunzi wanamlundikamano katika vyumba vya madarasa na pia tunauhaba wa madawati hata hivi vyumba vya madarasa tisa vilivyopo ni chakavu kabisa pia uhaba wa walimu maana nina walimu 30 kati yao moja ni wakujitolea hivyo walimu waliopo hawaendani na ikama ya wanafunzi waliopo jambo linapelekea kushuka kwa ufaulu shuleni hapa” amesema mwalimu mkuu

Majengo chakavu ya vyumba vya madarasa ya shule ya msingi michese

Awali akimkaribisha mkuu wa mkoa wa dodoma kuzungumza na wanafunzi wa darasa la Saba mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini JABIR SHEKIMWER amesema kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa vilivyopo atachangia mifuko mia moja ya saruji ili waweze kufyatua matofali waweze kuanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo.

wanafunzi wakiwa madarasani na wengine kukaa chini kwa ukosefu wa madawati

Mkuu wa mkoa wa Dodoma ANTONY MTAKA akizungumza na wanafunzi na wazazi shuleni hapo amemuagiza mkulugenzi mtendaji wa jiji la Dodoma kushulikia changamoto hizo zilizo elezwa na mwalimu mkuu wa Shule hiyo kwakuwa serikali imeshapitisha bajeti ya elimu hivyo katika fedha watakazo pokea wahakikishe wanaifikia shule hiyo ya michese kwa kuikarabati miundombinu ya majengi na Nyumba za walimu ikiwemo na ujenzi wa vyoo vya walimu shuleni hapo

Aidha MTAKA akawashukia wazazi na waridhie kuacha kuwapa watoto majukumu mengi ya kazi za nyumbani na badala yake kuwaachia muda mrefu wakiwa nyumbani wapate muda mwingi wa kujisomea kwakuwa elimu ndio msingi wa maisha yao.

“Hapa Kuna baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakiwatumikisha watoto kufanya kazi za nyumbani Kama kuosha vyombo, kufua,kuchota maji na kuwafanya watoto kuchoka muda mwingi na kushindwa kupata muda wa kujisomea wakiwa nyumbani na hili niwaambie wazazi wenzangu hasa wenye watoto wa madarasa ya mitihani Kama darasa la nne na la Saba na kidatu cha pili,nne na kidatu cha sita hakikisheni mnawapunguzia watoto majukumu ya kazi wakiwepo majumbani ili waweze kupata muda mwingi wakijisomea kwakuwa hakuna urithi mkubwa kwa mtoto Kama elimu” alisisitiza Mtaka

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mh ANTONY MAVUNDE amesema kutokana na changamoto hizo zilizopo shuleni hapo amewaomba kamati ya shule kujadili kwa kina changamoto hizo na na kumpelekea kipao mbele wanacho kiitaji ili Naye kwa kupitia mfuko wa Jimbo aweze kuchangia kama alivyochangia awali madawati hamsini na sasa Bado anatakiwa kuchangia pia katika ujenzi wa Choo cha walimu shuleni hapo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »