Na Barnabas Kisengi -Dodoma CHAMA cha Mapinduzi kimeziagiza Serikali mbili ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Zanzibar kupitia ilani ya uchaguzi Ibara namba 18 na 20wakati maelekezo ya Rais yakifanyiwa kazi nazo zifanye upya mapitio ya sera na Sheria za kodi ili kuliweka vyema suala hilo la tozo katika utekelezaji wake. Kauli hiyo imetolewa
Na Barnabas Kisengi -Dodoma
CHAMA cha Mapinduzi kimeziagiza Serikali mbili ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Zanzibar kupitia ilani ya uchaguzi Ibara namba 18 na 20wakati maelekezo ya Rais yakifanyiwa kazi nazo zifanye upya mapitio ya sera na Sheria za kodi ili kuliweka vyema suala hilo la tozo katika utekelezaji wake.
Kauli hiyo imetolewa hii leo Jijini Dodoma na Katibu wa itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka wakati alipokuwa akizu gumza na waandishi wa habari.
Sanjari na hilo Chama hicho kimempongeza Rais Samia Sluhu Hassan ka hatua ya kusitisha tozo ya miamala ya simu kwa lengo la kuwajali wananchi maskini.
Aidha katika hatua nyingine chama hicho kimempongeza Sheha Mpemba Faki kuwa Mbunge wa Jimbo la Konde Wilaya ya Micheweni Zanzibar baada ya kushinda uchaguzi Uliofanyika Julai 18 Mwaka huu ambaye alipata kura 1796 huku mgombea Mwenzie Mohamed Issa wa Chama cha ACT Wazalendo akipata kura 1373.
Hata hivyo katibu huyo amesema kuwa Chama Chama cha Mapinduzi (CCM )kimejipambanua katika Ilani yake ya uchaguzi ya Mwaka 2020/2025 kuhakiksha inawaletea wananchi maendeleo.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *