Joe Biden: Athibitishwa mshindi baada ya kura kuhesabiwa tena Georgia

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amethibitishwa kushinda uchaguzi Georgia baada ya kura kuhesabiwa tena, huku juhudi za kisheria za washirika wa Donald Trump kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo matatu zikitupiliwa mbali. Biden wa Democratic alimshinda mpinzani wake Trump wa Republican katika jimbo la Georgia kwa kura 12,284, kwa mujibu wa ukaguzi unaohitajika na

JOE BIDEN

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amethibitishwa kushinda uchaguzi Georgia baada ya kura kuhesabiwa tena, huku juhudi za kisheria za washirika wa Donald Trump kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo matatu zikitupiliwa mbali.

Biden wa Democratic alimshinda mpinzani wake Trump wa Republican katika jimbo la Georgia kwa kura 12,284, kwa mujibu wa ukaguzi unaohitajika na sheria ya mamlaka ya majimbo.

Bwana Biden alisema Trump alijua kwamba atashindwa na ameonesha “kutowajibika” kwa kukataa kukubali matokeo.

Mwanasiasa huyo wa chama cha Democratic anajiandaa kuingia madarakani mwezi Januari kama rais wa 46 wa Marekani.

Ushindi wa Bwana Biden unaonesha alipigiwa kura zaidi ya milioni 5.9. Katika mfumo wa uchaguzi kupitia wajumbe maalum, ambao unaamua ni nani atakuwa rais, Biden alipata kura 306 dhidi ya 232 – zaidi ya 270 alizohitaji kushinda.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »