NAIBU WAZIRI KIPANGA AFURAHISHWA NA MAENDELEO YA DIT-MWANZA

NAIBU WAZIRI KIPANGA AFURAHISHWA NA MAENDELEO YA DIT-MWANZA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Juma Kipanga (MB) leo tarehe 22 Julai, 2021 ametembelea Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Mwanza na kueleza kufurahishwa na maendeleo yaliyofikiwa, ikiwemo ujuzi wa wanafunzi kutengeneza bidhaa mbalimbali za ngozi. Miongoni mwa bidhaa alizoshuhudia katika Kampasi hiyo ni pamoja na viatu

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Juma Kipanga (MB) leo tarehe 22 Julai, 2021 ametembelea Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Mwanza na kueleza kufurahishwa na maendeleo yaliyofikiwa, ikiwemo ujuzi wa wanafunzi kutengeneza bidhaa mbalimbali za ngozi.


Miongoni mwa bidhaa alizoshuhudia katika Kampasi hiyo ni pamoja na viatu vya wanafunzi, jeshi na ofisini, mikanda pamoja na mikoba.


“Nimefurahishwa na maendeleo haya na sasa Serikali inajipanga kuweka miundombinu mipya ili tuondokane na teknolojia za zamani na hivyo kuongeza thamani katika mazao ya ngozi” amesema Naibu Waziri.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Kipanga aliambatana na Mkuu wa wilaya, Hassan Masala akiwa na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »