UVCCM YALAANI KAULI YA ASKOFU GWAJIMA JUU YA CHANJO YA CORONA

UVCCM YALAANI KAULI YA ASKOFU GWAJIMA JUU YA CHANJO YA CORONA

Na Barnabas Kisengi JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa  Chama cha Mapinduzi(UVCCM)Taifa umelaani vikali kauli za Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima za kupinga chanjo ya Corona huku ikiomba uongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM,kumchukulia hatua kali na  za kinidhamu. Kauli hiyo imetolewa hii leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo,Kenan Kihongosi

Na Barnabas Kisengi

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa  Chama cha Mapinduzi(UVCCM)Taifa umelaani vikali kauli za Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima za kupinga chanjo ya Corona huku ikiomba uongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM,kumchukulia hatua kali na  za kinidhamu.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo,Kenan Kihongosi wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mambo mbalimbali waliyojadiliana katika kikao cha sekretarieti kuhusina na Jumuiya hiyo.

Amesema  kuwa utaratibu wa chama kama mbunge ana hoja anatakiwa kuipeleke kwenye uongozi wa Chama kuliko kuongea sehemu nyingine huku akitaka viongozi wa Dini kutoa mahubiri ambayo yatawasaidia wananchi na kwamba huo ni utovu wa nidhamu.

Aidha amesema kama umoja wa Vijana wataendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa  Serikali ya awamu ya sita ya hivyo wananchi wasirubunike kwani lengo la Serikali ni kulinda Afya za wananchi Wabunge na viongozi wa Serikali na Chama wanaokinzana na masuala ya Serikali waache mara moja .

Hatua ya Jumuiya hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima kutoa mahubiri kwenye Kanisa lake la ufufuo na uzima lililopo Kawe Dar-es-Salaam akidai chanjo ya corona haifai na huenda ikawa na madhara kutokana na alichokieleza kuwa chanjo hiyo bado haijafanyiwa utafiti wa kutosha.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »