Serikali Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuondoa matukio ya ukatili wilayani humo.

Dodoma. Serikali Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuondoa matukio ya ukatili wilayani humo. Akizungumza katika kongamano la wasichana lililoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (Children’s Dignity Forum CDF) wilayani humo ambalo limewakutanisha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari ,Mkuu wa  Wilaya hiyo Jabir Shekimweri amesema

Dodoma.

Serikali Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuondoa matukio ya ukatili wilayani humo.

Akizungumza katika kongamano la wasichana lililoandaliwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (Children’s Dignity Forum CDF) wilayani humo ambalo limewakutanisha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari ,Mkuu wa  Wilaya hiyo Jabir Shekimweri amesema serikali inatambua umuhimu na ulazima wa  kushirikiana na wadau hao ili kuondoa vitendo hivyo.

Wakati huo huo amesema hawatosita kuwachukulia hatua wale wote watakao patikana na hatia kutenda vitendo hivyo huku akiwataka watendewa wa vitendo vya ukatili kutokuwalinda wahalifu ambao wamewatendea ukatili huo.

Katika hatua nyingine Shekimweri amewataka wanafunzi hao kujiepusha na vishawishi ambavyo husasabisha wengi kukatisha masomo yao kutokana na kupata ujauzito huku akitoa takwimu ya mimba  za wanafunzi wilayani humo amesema.

Kwa upande wake Meneja Utekelezaji wa Miradi Shirika la Jukwaa la Utuu wa Mtoto Bwana Evance Rwamuhuru amesema kongamano hilo limetoa fursa kwa wasichana ambao walikatisha masomo yao kutokana na kupata ujazito wakati wakiwa shule lengo likiwa ni kutoa funzo kwa wasichana ambao bado wanaendelea na masomo yao ni kipiti cha kujifunza kutoka kwao.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Wilayani humo ,Afisa Tarafa Olbert Mwalyego amesema ni muhimu wanafunzi hao wakazingatia masomo yao ili waweze kutimiza  malengo waliojiwekea na kukataa vishawishi ambavyo vimekuwa vikiwaharibia ndoto zao za baadae.

Mwakilishi wa wanafunzi wilaya ya mpwapwa  Aveline Madanya wa  kitato cha tatu shule ya Sekondari Mount Igovu amesema miongoni mwa changamoto zinazowakumba wanafunzi wilayani humo ni mimba za utotoni ,wazazi kutowapatia mahitaji watoto wao,umbali mrefu,kutokuwa na elimu juu ya masuala ya uzazi pamoja na vishawishi vinavyopelekea wanafunzi kupata mimba wangali shule.

Hatahivyo,Serikali Wilayani humo imesema si vyema kwa wananchi kuendelea kufumbia macho vitendo vya ukatili wa  kijinsia ambavyo hutokea  katika maeneo yao badala yake vinapaswa kutolewa taarifa katika vyombo husika ili hutua ziweze kuchukuliwa kwa walifu wa vitendo hivyo.


Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »