LUSINDE AWATAKA WABUNGE KUSIMAMIA FEDHA ZA MIRADI KWA WELEDI

LUSINDE AWATAKA WABUNGE KUSIMAMIA FEDHA ZA MIRADI KWA WELEDI

Na Barnabas Kisengi, DODOMA Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa (MNEC) na Mbunge wa Jimbo la Mvumi mkoani Dodoma Mhe Livingstone Lusinde amewaomba Wabunge kusimamia fedha walizopewa za kujenga barabara katika majimbo yao ambayo fedha hizo zimeelekezwa kwa wakala wa barabara za mijini na vijijini  (TARURA) kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo. Akizungumza na waandishi wa

Na Barnabas Kisengi, DODOMA

Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa (MNEC) na Mbunge wa Jimbo la Mvumi mkoani Dodoma Mhe Livingstone Lusinde amewaomba Wabunge kusimamia fedha walizopewa za kujenga barabara katika majimbo yao ambayo fedha hizo zimeelekezwa kwa wakala wa barabara za mijini na vijijini  (TARURA) kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Mhe Livingstone Lusinde amesema kuwa katika bajeti iliyopita kila Mbunge wa jimbo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepatiwa kiasi cha fedha zaidi ya Bilion moja kwaajili ya barabara katika majimbo yote nchini.

Aidha,Mhe Lusinde amewasihi watanzania kutoingilia muhimili wa mahakama kawni mahakama ni chombo huru ambacho kinatoa haki kwa kila mtu huku akiwaomba watanzania kuendelea kuikumbatia amani iliyopo nchini.

Hata hivyo Mhe Lusinde amebainisha kuwa wao kama wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanakatwa kodi ambazo zinaenda kwenye shughuli za kimaendeleo hapa nchini hivyo jamii iondokane na maneno ya watu kutokusema kuwa wabunge hawakatwi kodi  mfano mimi kama lusinde mbunge wa jimbo la mvumi ninapokea mshahara wa halali shilingi milioni 4.6 na mshahara wangu unakatwa kodi mbalimbali na makato yote ninayokatwa yanafikia kiasi cha shingi milioni 1.2 kwa mwezi sasa watanzania tambueni wabunge wote tunakatwa kodi ambazo zinaenda kwenye shuguli za maendeleo hapa nchini pia amesema kuwa jamii iunge mkono shughuli zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais samia suluhu Hassan.

Sambamba na hayo Mhe Lusinde amempongeza RAIS SAMIA SULUH HASSAN kwa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo hapa nchini kwa manufaa ya watanzania na amewaasa watanzania kuendelea kuchukua tahadhali ya ugonjwa wa uviko 19 kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na serikali na wizara ya afya

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »