KIHONGOSI AMVAA PAMBALU “kuwa na adabu, heshimu Sheria za Nchi”

KIHONGOSI AMVAA PAMBALU “kuwa na adabu, heshimu Sheria za Nchi”

Na Barnabas Kisengi, DODOMA KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kenan  Kihongosi amemvaa  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) John Pambalu kwa kumtaka   kuwa na adabu na kuheshimu sheria za Nchi huku akiwataka watanzania kutoandamana Julai 5 mwaka huu. Hatua hii imekuja

Na Barnabas Kisengi, DODOMA


KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kenan  Kihongosi amemvaa  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) John Pambalu kwa kumtaka   kuwa na adabu na kuheshimu sheria za Nchi huku akiwataka watanzania kutoandamana Julai 5 mwaka huu.


Hatua hii imekuja kufuatia Mwenyekiti huyo wa Bavicha kutoa tamko   kuwataka  Vijana wa Chama hicho kuandamana Agosti 5  kwa madai ya kudai demokrasia kuhusu kesi inayomkabili  Mwenyekiti wao Freeman Mbowe.


Akizungumza leo Agosti 3,2021,Katibu Mkuu huyo wa UVCCM amesema kuwa ni aibu kwa watu wazima kuendelea kung’ang’ania mambo ambayo hayawezekani huku akiwataka kufuata taratibu za mahakama ambapo  amedai  hakuna mtu aliye juu ya sheria na hakuna mwenye  mamlaka ya kumtaka Mheshimiwa  Rais kufanya jambo au matakwa yao binafsi.


Katibu huyo ameeleza kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA lazima atambue kwamba nchi hii inaongozwa na Sheria na kwamba siku zote wao wamekuwa wakijipambanua kuwa wanataka Demokrasia Sasa anashangaa wanataka kuvunja Sheria na kusahau kuwa kila mhimili unafanya kazi kwa namna yake.
“Mnapotaka kuandamana kupinga kuhusu yanayomhusu Mbowe mmejiridhisha vipi kwamba hana makosa,mna wajibu wa kutii sheria za nchi,”amesema.


Kihongosi amewataka Wanachama hao wanaotaka  kuandamana kuendelea kufanya shughuli za Maendeleo kwa ajili ya manufaa kwa  familia zao badala ya kutumia muda huo kwa masuala yasiyo na msingi.
“Niwashauri tu vijana wenzangu, badala ya kuandamana muda huo tumieni kutafuta ugali wa familia zenu.Wapinzani wanapaswa wajitafakari ,wabadilike na kukubali kubadilisha  aina ya Mfumo wa siasa wanaoutumia ,lazima katika siasa kuna ushindani,wahakikishe wanakuwa Mabalozi wa amani na kuepuka kuhamasisha vurugu,”amesema.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »