TUMEAZIMIA KUTOKOMEZA UGONJWA WA KIFUA KIKUU-DR ABEL MAKUBI

Na Barnabas Kisengi DodomaNovember  23 2020 Dodoma Serikali ya Tanzania imeazimia kutokomeza kabisa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuongeza uwezo wa ugunduzi wa wagonjwa wapya wa kifua kikuu na kuwaweka kwenye matibabu.Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu an Ukoma

Na Barnabas Kisengi DodomaNovember  23 2020

Dodoma 
Serikali ya Tanzania imeazimia kutokomeza kabisa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuongeza uwezo wa ugunduzi wa wagonjwa wapya wa kifua kikuu na kuwaweka kwenye matibabu.
Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu an Ukoma uliofanyika Jijini Dodoma.
“Uwezo wa nchi kugundua wagonjwa wapya na kuwaweka kwenye matibabu umeongezeka kutoka wagonjwa 62,908 (33%) mwaka 2015 na kwa sasa kufikia wagonjwa 82,166 (59%)” amesema Prof. Makubi
Kufuatia hatua hiyo Prof. Makubi amesema kuwa maisha ya wananchi takribani 300,000 ikiwemo ya watoto 45,000 yameponywa kwa kupatiwa dawa kwa wakati na kufuatiliwa kwa usahihi kuanzia mwaka 2015 hadi sasa.
Juhudi hizo pia zimeweka kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na kifua kikuu kwa 33%. “Mwaka 2015 kulikuwa na vifo 30,000 hivi sasa vimepungua hadi kufikia vifo 20,000” amesema Prof. Makubi.
Prof. Makubi amesema kuwa mafanikio hayo ya ongezeko la kasi ya ugunduzi wa wagonjwa wapya yametokana na mikakati mbalimbali iliyowekwa na Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma ikiwemo kuboresha huduma za ugunduzi wa TB na kutoa kipaumbele kwa makundi yaliyoathirika zaidi kama vile kaya zenye wagonjwa, wanaoishi kwenye kaya duni, gerezani, wachimbaji wadogo wadogo na kwa waathirika wa madawa ya kulevya.
“Aidha tumewekeza katika afua bunifu mbalimbali za matumizi ya teknolojia mpya za molekyula za kubaini TB kwa usahihi na kwa haraka” amesisitiza Prof. Makubi.
Awali akizungumza, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi amesema Wizara imefanya vizuri kwenye kwa kufikia malengo waliyoyaweka kwenye Mpango mkakati ambao unamalizika mwaka huu 2020.
“Malengo ambayo tulijiwekea ya kupunguza vifo vitokanavyo na kifua kikuu tumeweza kuyafikia pamoja na kupunguza madhaa yanayotokana na ugonjwa huo” amesema Dkt. Subi
Amesema kuwa Serikali imefanikiwa kuongeza vituo vya upimaji wa kifua kikuu sugu kutoka kituo 1 mwaka 2015 hadi kufika vituo 145 hivyo kuongeza wigo wa huduma za matibabu ya ugonjwa huo
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa Dkt. Ntuli Kapologwe amesema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana Wizara ya Afya katika kipindi cha miaka 5 ijayo imejiwekea mikakati ya kuwawezesha watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wawe na ujuzi na uwezo wa kutambua na kutoa huduma kwa wagonjwa wa kifua kikuu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »