“Shusheni bei za bidhaa kabla Serikali haijachukua hatua”.Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

“Shusheni bei za bidhaa kabla Serikali haijachukua hatua”.Makamu wa Pili wa Rais  Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Wafanyabiashara Nchini wametakiwa kuacha mara moja upandishaji wa bei za bidhaa  ili kuwapunguzia wananchi ukali wa maisha. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo katika kikao maalum kilichowakutanisha Viongozi wa wizara,wafanyabishara, na maafisa wa usimamizi wa Kodi kwa lengo la kulipatia ufumbuzi tatizo la upandaji wa Bei za Bidhaa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na vizongozi wa wizara pamoja na wafanyabiashara wa Zanzibar katika kulitafutia ufumbuzi tatizo la kupanda bei kwa bidhaa jambo ambalo linasababisha ugumu wa maisha kwa wananchi hasa wa kipato cha Chini.

Wafanyabiashara Nchini wametakiwa kuacha mara moja upandishaji wa bei za bidhaa  ili kuwapunguzia wananchi ukali wa maisha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo katika kikao maalum kilichowakutanisha Viongozi wa wizara,wafanyabishara, na maafisa wa usimamizi wa Kodi kwa lengo la kulipatia ufumbuzi tatizo la upandaji wa Bei za Bidhaa.

Mhe. Hemed alisema sio jambo linapendeza kwa wafanyabiashara kukiuka miongozo na taratibu zilizowekwa na serikali juu ya bei za bidhaa kutokana na upandishaji wa bei unasababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi hasa wale wa kipato cha chini.

Alieleza kuwa wananchi wamekuwa wakiitupia lawama serikali yao kwa kuona hakuna unafuu wa bidhaa hasa za chakula jambo linalosababishwa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu.

Katika kikao Hicho Makamu wa Pili wa Rais alilazimika kupiga simu kwa wauzaji wa bidhaa kutoka Nje ya Nchi ili kulinganisha gharama za bei wanazonunulia wafanyabiashara hao na bei wanazowauzia wananchi na kugundua kuwa kuna tofauti kubwa ya bei hizo.

Aliwataka wafanyabiashara hao kupunguza bei za bidhaa mara moja kabla serikali haijachukuwa hatua za kinidhamu dhidi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kwa kuwafutia kibali cha kufanya biashara Zanzibar.

Akichangia katika kikao hicho Waziri wa Biashara na maendeleo ya viwanda Mhe. Omar Said Shaaban alimuleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa na tabia ya kukacha kufuata miongozo inayowekwa na serikali katika udhaaji wa bei za bidhaa.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali alisema kuwa wananchi wa Zanzibar hawana jukumu la kuwachangia Mitaji wafabyabiashara katika kuendesha biasgara zao, hivyo suala la kupandisha bei za bidhaa bila ya kufuata taratibu halikubaliki.  

Nae, mfanyabisha maarufu Zanzibar Said Bopar aliwataka wafanyabishara wenziwe kuwa waaminifu kwa kuwaonea huruma wananchi kutokana na upatikanaji wa bidhaa hizo katika soko kuwa wa kuridhisha.

Katika kikao hicho kilichowakutanisha wadau kutoka sekta mbali mbali kimetoka na azimio kwa bei ya dumu moja la mafuta liuzwe kwa bei ya Shillingi Sabiini na Tano Elfu (75,000/=) kutoka Shilling Themanini na Mbili Elfu ikiwa ni tofauti ya shilling Elfu saba.

…………………………..

Kassim Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

09/08/2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »