TIGO NA SANLAM INSURRANCE WAZINDUA HUDUMA YA BIMA YA SIMU JANJA

TIGO NA SANLAM INSURRANCE WAZINDUA HUDUMA YA BIMA YA SIMU JANJA

Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania, imeshirikiana na kampuni ya Sanlam, kuanzisha bima ya simu janja (Smartphones). Huduma hii ni kwa simu mpya zinazonunuliwa katika maduka ya Tigo kote nchini. Mpango huu ni kwa ajili ya simu zinazopotea, kuharibika kwa bahati mbaya au kuibiwa Akizungumzia ushirikiano huo, Mkuu wa Maduka na Bidhaa za

Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania, imeshirikiana na kampuni ya Sanlam, kuanzisha bima ya simu janja (Smartphones). Huduma hii ni kwa

simu mpya zinazonunuliwa katika maduka ya Tigo kote nchini. Mpango huu ni kwa ajili ya simu zinazopotea, kuharibika kwa bahati mbaya au kuibiwa

Mkuu wa Maduka na Bidhaa za Tigo, Mkumbo Myonga

Akizungumzia ushirikiano huo, Mkuu wa Maduka na Bidhaa za Tigo, Mkumbo Myonga alisema, “Katika ulimwengu ambapo simu janja zimekuwa muhimu sana kwa watu wengi ambao huzitegemea kuwasiliana na dunia kupitia mitandao ya kijamii, huku wengine wakizitumia kama ofisi zao za kazi, ushirikiano huu na Sanlam utawapa bima wamiliki wa simu za mkononi endapo simu zao zitapotea au kuharibika”

“Mara baada ya wateja kununua simu kutoka kwenye maduka yetu, mbali na dhamana (warranty) ya kawaida, tunashauri wakatie bima simu janja zao mpya. Mpango huu unakidhi haja za wateja wetu, hususani wanaotaka kulinda simu zao zinazoharibika au kupasuka kwa bahati mbaya. Muda bima utakuwa ni miezi 12 (mwaka mmoja) ambapo mmiliki wa simu atatakiwa kulipa asilimia 5 ya jumla ya gharama ya kununulia simu yake ya mkononi kama malipo ya bima” Alieleza Mkumbo.

Wateja wanaweza kupata bima ya simu janja kwa kutembelea maduka ya Tigo yaliyopo nchi nzima. Kwa maelezo zaidi, wateja wanaweza kutembelea tovuti ya www.tigo.co.tz au kupiga simu bure kwenda namba 0800 714 447.

Akiwa katika tukio la uzinduzi, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Sanlam, Geofray Masige alisema, mpango huu wa bima, utahakikisha kuwa wateja wa Tigo wanatengenezewa au kurudishiwa simu zao haraka baada ya kuharibika au kupotea ndani ya muda uliowekwa.

Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Sanlam, Geofray Masige

“Simu janja sasa imekuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ya wanadamu. Ukiachia mbali gharama halisi ya kununulia, kifaa hiki kina thamani kubwa kwa mtumiaji wake na hofu ya kupoteza ni kubwa kwa watu wengi, lakini kwa hili Sanlam na Tigo tumeleta suluhisho,” alisema.

Masige aliongeza kuwa, mpango huu wa bima ya simu za mkononi ni nafuu sana na kujiandikisha ni rahisi sana, maana hakuna kutumia makaratasi, bali taarifa zote za mteja zitahifadhiwa kidijitali. Mteja atalipwa madai yake ya fidia ndani ya siku 14 huku madai ya simu iliyoibiwa yakichukua mpaka siku 7 tu baada ya kuwasilisha nyaraka zote zinazohitajika.

Taarifa zaidi pia zinapatikana kupitia ofisi zote za Sanlam jijini Mwanza, Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Mbeya.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »