KIHONGOSI AWATAKA VIJANA WAJIAJIRI BADALA YA KUSUBIRI AJIRA SERILALINI

KIHONGOSI AWATAKA VIJANA WAJIAJIRI BADALA YA KUSUBIRI AJIRA SERILALINI

Na Barnabas Kisengi, Dodoma. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)  KENAN KIHONGOSI amewataka vijana kuacha kubweteka  na kusubiri ajira zinazotolewa na serikali na badala yake wajikite kwenye kujiajiri wenyewe kwa kufanya kazi za ujasiliamali ili waweze kujikwimu kimaisha. Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakiti akiwa kwenye kikao na

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)  KENAN KIHONGOSI

Na Barnabas Kisengi, Dodoma.


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)  KENAN KIHONGOSI amewataka vijana kuacha kubweteka  na kusubiri ajira zinazotolewa na serikali na badala yake wajikite kwenye kujiajiri wenyewe kwa kufanya kazi za ujasiliamali ili waweze kujikwimu kimaisha.


Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakiti akiwa kwenye kikao na makatibu wa umoja wa vijana wa mikoa waliokutana jijini dodoma kujadili maendeleo ya umoja huu wa vijana hapa nchini.
“Vijana wengi wamekuwa wakimaliza vyuo na kusubiri kuajiriwa na serikali jambo ambalo linakuwa gumu kwa vijana wote wanao maliza vyuo na kupata ajira sasa sisi kama viongozi waliotuamini kuwaongoza tumeamua kuweka mfumo wa kuanzisha kongamano ambalo litawapa fursa vijana wengi kuzungumzia changamoto zao ili tuwawekee mfumo wa kujifunza ujasiliamali ili waweze kujiajiri wenyewe kwani vijana ni kundi kubwa hapa nchini” amesema Kihongosi.


Aidha kihongosi amewataka vijana kuacha kutumia muda mrefu kwenye mitandao ya kijamia kujadili mambo yasiyo na msingi na kuwa na tabia ya kuchafuana kwenye mitandao badala yake watumie mitandao ya kijamia kusemea mazuri yanayotekelezwa na serika ya awamu ya sita inayoendelea kukamilisha miradi mikubwa na yakimkakati inayotekelezwa hapa nchi kwa kupitia tozo mbalimbali zinazoendelea kukusanywa.
“Hivi karibuni tumesikia waziri wa fedha na mipango kwa kushirikiana na waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa wamesema wamefanikiwa kukusanya tozo ya shilingi bilion 48.4 ambazo fedha hizo zimeelekezwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini ambapo inakwenda kujenga vituo vya afya 150 na vyumba vya madarasa 500″amesema kihongosi


Aidha katibu wa umoja wa vijana (UVCCM) KENAN KIHONGOSi amewataka watendaji wa serikali hasa katika halmashauri ambapo fedha hizo zimeelekezwa katika ujenzi wa vituo vya afya na vyumba vyumba vya madarasa kuhakikisha wanazitumia vizuri fedha hizo na kuonyesha samani ya fedha hizo ambazo ni kadi za wananchi.


Kihongosi amesema hivi karibuni wanatarajia kuanzisha ligi ya mashindano mbalimbali  kwa vijana hapa nchini ili kuhakikisha wanakuza vipaji mbalimbali katika michezo mbalimbali pia michezo ni ajira na amewataka vijana kuhakikisha wanaendelea kulinda amani ya nchi na kuwa waadilifu na wazalendo  wa nchi yetu ya Tanzania


Katibu kihongosi amesema umoja wa vijana unampongeza RAIS SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na nchi mbalimbali ambazo amezitembelea kama vile kenya ambapo kulikuwa na mgogoro wa wafanyabiashara ambapo baada ya kufanya ziara nchini kenye waliweza kumaliza mgogoro huo wa wafanyabiashara na sasa nchi hizi zinaendelea vizuri katika biashara.


Aidha kihongosi amesema kuwa RAIS Amekuwa akifanya ziara mbalimbali kujenga demokrasia ya nchi ambamo hivi karibuni RAIS amefanya ziara katika nchi ya uganda,rwandwa,malawi na leo ameelekea nchini zimbwabwe kwenda kushuhudia kuapishwa kwa RAIS wa nchi hiyo MHE. RAIS HAKAINDE HICHILEMA.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »