Rashid Charles Mberesero:Mtanzania aliyefungwa kwa ugaidi Kenya ajinyonga gerezani.

Mtanzania aliyehukumiwa kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi lililotokea mwaka 2015 katika chuo kikuu kimoja nchini Kenya na kusababisha watu 148 kufariki , amejiua mwenyewe akiwa gerezani , vyombo vya habari vya Kenya vimeripoti. Washambuliaji wanne waliuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Kenya katika chuo kikuu cha Garissa ,lakini Rashid Charles Mberesero, na wenzake

kenya
Rashid Charles Mberesero.

Mtanzania aliyehukumiwa kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi lililotokea mwaka 2015 katika chuo kikuu kimoja nchini Kenya na kusababisha watu 148 kufariki , amejiua mwenyewe akiwa gerezani , vyombo vya habari vya Kenya vimeripoti.

Washambuliaji wanne waliuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Kenya katika chuo kikuu cha Garissa ,lakini Rashid Charles Mberesero, na wenzake wawili walikamatwa na mwaka jana walihukumiwa kwa kuhusika katika ugaidi.

Hukumu hiyo ilimpa bwana Mberesero kifungo cha maisha gerezani,Taarifa zinasema alikuwa na matatizo ya akili wakati akiwa gerezani na alikuwa anamuona mtaalamu wa afya akiwa gerezani.

Gazeti la Daily Nation linasema Mberesero alijinyonga mwenyewe akiwa gerezani kwa kutumia blanketi lake,

Shambulio kubwa kutokea mwaka 2015 liliacha simanzi kubwa nchini Kenya.

Al-Shabab ilisema imekuwa katika vita na Kenya tangu askari wa Kenya kuingia Somalia mnamo Oktoka 2011.

BBC. SWAHILI.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »