MAMA WA KAMBO JERA KWA KUMSHAMBULIA MTOTO WA MUME WAKE

Mahakama ya wilaya ya Kigoma imemuhukumu Agness Damian( 40)mkazi wa Mji mwema manispaa ya Kigoma Ujiji kwenda jela miaka miwili na kulipa fidia ya shilingi milioni tano kwa kosa la kumshambulia na kumkatakata kwa wembe mtoto wa mme wake mwenye umri wa miaka 15. Kesi namba 95 ya mwaka 2020 dhidi ya Agness Damian inadaiwa

Mahakama ya wilaya ya Kigoma imemuhukumu Agness Damian( 40)mkazi wa Mji mwema manispaa ya Kigoma Ujiji kwenda jela miaka miwili na kulipa fidia ya shilingi milioni tano kwa kosa la kumshambulia na kumkatakata kwa wembe mtoto wa mme wake mwenye umri wa miaka 15.

Kesi namba 95 ya mwaka 2020 dhidi ya Agness Damian inadaiwa kosa hilo alilitenda mnamo 18 June,2020 baada ya mwanamke huyo kumtuhumu aliyejeruhiwa na tukio hilo kuwa amempiga mdogo wake ambaye ni mtoto wake

Inaelezwa mshtakiwa alitekeleza  ukatili huo na kumsababisha muhanga kupata majeraha na  kulazwa hospitali kwa siku nane akifanyiwa matibabu

Eva Mushi  hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya kigoma amesema mahakama imepitia na kuridhishwa na  ushahidi upande wa mashtaka uliojumuisha mhanga wa tukio hilo,mama mzazi wa mtoto na baba mzazi wa mtoto huyo ,jirani ,Daktari na ushahidi wa polisi.

Hivyo mahakama imemtia hatihani kwa mujibu wa kifungu cha 225 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 marejeo ya mwaka 2019 mahakama imemtia hatiani na kumuhukumu kwenda jela miaka miwili na fidia ya milioni tano.

kabla ya hukumu mshtakiwa alipotakiwa kujitetea  aliomba mahakama impunguzie adhabu  kwani yeye ni yatima na anategemewa na watoto wawili na kati yao mmoja akiwa na umri mdoogo

 CUTS…MAMA WA KAMBO JELA.mp4

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »