Morogoro yajipanga ujenzi vyumba vya madarasa, RC atoa utaratibu mpya

Morogoro yajipanga ujenzi vyumba vya madarasa, RC atoa utaratibu mpya

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amewataka Wakurugenzi Watendaji na Madiwani wa Halmashauri zote Mkoani humo kuwa na utaratibu wa kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wananfunzi wa kidato cha kwanza kila ifikapo mwezi Julai ili kuondokana na mazoea ya kukimbizana na ujenzi huo inapofika mwezi Desemba kila mwaka. Martine Shigela

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amewataka Wakurugenzi Watendaji na Madiwani wa Halmashauri zote Mkoani humo kuwa na utaratibu wa kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wananfunzi wa kidato cha kwanza kila ifikapo mwezi Julai ili kuondokana na mazoea ya kukimbizana na ujenzi huo inapofika mwezi Desemba kila mwaka.

Martine Shigela ametoa maagizo hayo wakati wa kikao cha kujadili namna ya kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kupokelewa mwezi Januari 2022 kilichofanyika katika ukumbi wa CCT uliopo Kilakala katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Amesema, viongozi wote wanajua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa na miundombinu mingine ambayo hujitokeza kila mwaka lakini bado viongozi hao husubiri maelekezo ya viongozi wa Serikali kutoka juu na ikifika mwezi Disemba kuanza kukimbizana kwa ajili ya kutekeleza maagizo hayo kama vile hawajua uwepo wa changamoto hiyo.

Kwa sababu hiyo, Martine Shigela ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kujipanga katika kukabiliana na upungufu wa madarasa kila ifikapo Mwezi Julai ili ifikapo mwezi Disemba changamoto hiyo iwe imetatuliwa.

“Kwa nini hatujipangi kuanzia Julai tukaanza kujenga kidogo kidogo kwa nguvu za wananchi na Halmashauri yenyewe, sasa hivi tupo mwezi wa nane tunaingia wa tisa, tuna miezi mitatu ya kujipanga vizuri ili matokeo yakitoka jambo hili liwe limekamilika..” alisisitiza Mhe. Shigela..

Naye Katibu Tawala Msaidizi upande wa Mipango na Uratibu Anza Amen Ndossa amesema, kutokana na upungufu wa madarasa 428, Mkoa unalazimika kuanza mapema kuunganisha nguvu na kuhamasisha wananchi na wadau wengine wa Elimu kujenga vyumba hivyo 428 vya madarasakwa shule za Sekondari kabla ya mwezi Disemba, 2021.

‘’Tusipojipanga mapema baadhi ya wanafunzi watashindwa kujiunga na Kidato cha kwanza kwa kukosa vyumba vya Madarasa’’ Amesema Ndossa.

Alibainisha mkoa wa Morogoro  unakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 428 kwa ajili ya wanafunzi 25,300 wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kupokelewa mapema mwezi Januari 2022  

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wajumbe wa kikao hicho wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri  na baadhi ya Madiwani pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri, licha ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa kuja na utaratibu wa kuanza maandalizi ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa mapema, wamemuahidi kutekeleza maagizo hayo aliyoyatoa ili kuondokana na changamoto hiyo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »