WAHANDISHI 630 KULA KIAPO CHA UTII JIJINI DODOMA

WAHANDISHI 630 KULA KIAPO CHA UTII JIJINI DODOMA

NA PENDO MANGALA,DODOMA. WAHANDISI wataalamu 630, wanatarajia kula kiapo cha utii wa taaluma yao ili kuhakikisha kuwa wanawajibika vyema katika taaluma zao, ambapo kiapo hicho hicho kitatumiwa na vyombo mbalimbali kuwawajibisha pale watakapo kiuka sheria na taratibu katika majukumu yao kila siku.Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano mkuu

NA PENDO MANGALA,DODOMA.


WAHANDISI wataalamu 630, wanatarajia kula kiapo cha utii wa taaluma yao ili kuhakikisha kuwa wanawajibika vyema katika taaluma zao, ambapo kiapo hicho hicho kitatumiwa na vyombo mbalimbali kuwawajibisha pale watakapo kiuka sheria na taratibu katika majukumu yao kila siku.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano mkuu wa Bodi ya usajili Wahandisi nchini (ERB) Prof, Bakari Mwinyiwiwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Wahandisi Tanzania mwaka 2021.
Prof.Mwinyiwiwa amesema maadhimisho hayo yamepangwa kufanyika jijini Dodoma kwa siku mbili Alhamisi ya Septemba mbili hadi ijumaa Septemba 03 mwaka huu katika ukumbi wa Jakaya Kiwete.


Amesema katika majadiliano kitaaluma mada kuu itakuwa ni athari za mapinduzi ya nne ya viwanda kwenye miundombinu na viwanda kwa uendelevu wa uchumi wa kati huku akiongeza kwamba kutakuwa na mada zingine ndogondogo ikiambatana na utaoji wa tuzo



Kwa upande wake Msajili Bodi ya usajili Wahandisi nchini Patrick Barozi, amesema kuwa hadi sasa wahandisi 17, wamechukuliwa hatua za kinidhamu kwa makosa mbalimbali.

Aidha bodi imewasihi wahandisi nchini kushiriki katika maadhimisho ya siku ya wahandisi huku ikiwaomba waajiri wote kuwaruhusu na kufadhiri ushiriki wa wahandisi wao ili waweze kushiriki mwelekeo wa nchi katika mapinduzi ya teknolojia.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »