Na Barnabas Kisengi-Dodoma Mamlaka ya Uthibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kupanda kwa bei za mafuta nchini kuanzia Semptemba 01 2021 kwa bei za mafuta ya petroli, Dizeli na mafuta ya taa Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkuu wa kitengo cha mahusiano na habari Titus Kaguo amesema kuwa Ewura imetangaza kupanda kwa
Na Barnabas Kisengi-Dodoma
Mamlaka ya Uthibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kupanda kwa bei za mafuta nchini kuanzia Semptemba 01 2021 kwa bei za mafuta ya petroli, Dizeli na mafuta ya taa
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkuu wa kitengo cha mahusiano na habari Titus Kaguo amesema kuwa Ewura imetangaza kupanda kwa bei hizo za mafuta kuanzia septemba 01 2021 hapa nchini.
Kaguo amesema kwa Bandari ya Dar es Salaam bei imepanda kwa mafuta ya petroli Tsh 84, dizeli Tsh 39 na mafuta ya taa Tsh 18 na kwa bandari Tanga petroli ni Tsh 53, dizeli 14 na kwa bandari ya Mtwara petroli imepanda kwa Tsh 108 na dizeli imepanda kwa Tsh 46
Aidha kaguo amesema bei hiyo ndiyo itaanza kutumika kesho na amewataka wananchi wanaotumia nishati ya mafuta kuhakikisha hawauziwi zaidi ya bei iliyoelekezwa na EWURA na pindi watakapoona bei imezidi watoe taarifa kwa vyombo husika.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *