WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA ASKARI MAGEREZA KUACHA KUWATESA WAFUNGWA

WAZIRI SIMBACHAWENE AWATAKA ASKARI MAGEREZA KUACHA KUWATESA WAFUNGWA

Na Barnabas Kisengi,Dodoma  WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi George Simbachawene amelitaka Jeshi la Magereza nchini kuacha kuwafunga wafungwa kikoroni kwa kuwatesa na kuwanyima haki zao za msingi na badala yake kutumia wafungwa hao kama nguvu kazi  ya kuleta mafanikio magerezani.Amesema Jeshi ni sehemu ya kujifunza hivyo watumie sehemu hiyo kuwarekebisha,kuwafundisha kuwa raia wema

Na Barnabas Kisengi,Dodoma 


WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi George Simbachawene amelitaka Jeshi la Magereza nchini kuacha kuwafunga wafungwa kikoroni kwa kuwatesa na kuwanyima haki zao za msingi na badala yake kutumia wafungwa hao kama nguvu kazi  ya kuleta mafanikio magerezani.
Amesema Jeshi ni sehemu ya kujifunza hivyo watumie sehemu hiyo kuwarekebisha,kuwafundisha kuwa raia wema hata wanaporejea katika jamii waonekane jeshi limefanya kazi nzuri.


Simbachawene ameyasema hayo Leo  jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano  wa siku tatu wa Maafisa waandamizi wa jeshi la Magereza wenye lengo la   kujadili changamoto wanazokumbana nazo, na tathimini  ya shughuli zinazofanywa na jeshi la Magereza.
Amesema  wafungwa wengi wamekuwa wakinyimwa haki zao za msingi wanapokua gerezani ikiwemo kulala,kubadilisha nguo,na kula kwa wakati na kusahau kuwa mfungwa ndio rasilimali mtu katika gereza.


“Ni ukweli usiopingika Jeshi hili mmejitahidi sana endeleni kuwa wabunifu  wa miradi mbalimbali pia tumieni hawa wafungwa kama rasilimali watu,lindeni mafanikio haya  ili yalete matunda” amesema Simbachawene
Pia amelipongeza Jeshi hilo kwa kuweza kujitegemea kwa kufungua miradi mingi ya ubunifu  ikiwemo ujenzi wa nyumba za makazi ya maafisa na askari,ujenzi wa makao makuu ya jeshi, ununuzi wa vitendea kazi, hali iliyopelekea kuondokana na utegemezi.


Kwa upande wake Kamishina Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee amewataka maafisa hao kutumia mkutano huo kujadili na kuleta maendeleo katika maeneo wanayo simamia kuimarisha sekta ya kilimo.
“Tumefanikuwa kutembea maeneo yote nchini kasoro Kisiwa cha Mafia na Mkoa wa Iringa kwa kuwa na utekelezaji hasa katika kujenga mabweni ya wafungwa na miradi mingi inayoendelea nchini,magari,mashine,mikopo,kampuni ya ulinzi pamoja na viwanda “amesema Mzee
Waziri Simbachawene ameweka jiwe la msingi katika sehemu ya kutengenezea mikate (Bakery) , Kisima cha maji na nyumba 34 za maafisa askari wa makao makuu ambapo maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemyo ” Fikra mpya, mtazamo mpya kufanyakazi kwa bidii na kujitegemea”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »