DC SHEKIMWERI AWATAKA WAFANYAKAZI WA DUWASA KUWA WAAMINIFU, WAZALENDO NA WAADILIFU

DC SHEKIMWERI AWATAKA WAFANYAKAZI WA DUWASA KUWA WAAMINIFU, WAZALENDO NA WAADILIFU

Na Barnabas Kisengi Dodoma  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri amewataka wafanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Dodoma (DUWASA) kuiga nyayo za alikopita Mhandisi Mayunga kashilimu kwa kuwa waaminifu, wazalendo, wadilifu na kuwa na hofu ya mungu katika utumishi wao katika kazi zao siku zote wawatumikiapo wananchi Kauli

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri
Mhandisi Mayunga Kashilimu, Aliyekuwa Meneja Ufundi wa Duwasa

Na Barnabas Kisengi Dodoma 


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri amewataka wafanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Dodoma (DUWASA) kuiga nyayo za alikopita Mhandisi Mayunga kashilimu kwa kuwa waaminifu, wazalendo, wadilifu na kuwa na hofu ya mungu katika utumishi wao katika kazi zao siku zote wawatumikiapo wananchi


Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na jfivetv.com ya kumpa pongezi za dhati kwa aliyekuwa meneja ufundi wa Duwasa kwa kupandishwa cheo kuwa mkurugenzi mtendaji kwa utendaji wake wa kazi kuwa mzuri na wakizalendo.
Shekimweri amesema serikali ya awamu ya sita imeweka fedha nyingi katika miradi ya maji hapa nchini kwa kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani na kuhakikisha watanzania wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama hivyo kwa wataalamu wa duwasa wahakikishe wanatimiza wajibu wao wa kuhakikisha miradi inayotekelezwa jijini Dodoma inakamilika kwa wakati. 
“nikiangalia kwa wilaya ya Dodoma mjini ni duwasa mmefanya kazi nzuri japo bado kunamaeno yanachangamoto bado ya upatikanaji wa maji hivyo lazima kujipanga kuhakikisha changamoto hiyo mnaifanyia kazi ili wananchi wapate huduma vizuri na kuondokana na mgao na ukizingatia Dodoma sasa ndio makao makuu ya serikali hivyo mnapaswa kuongeza kasi katika utendajiwenu wa kazi”amesema Shekimweri.


“Pia angalieni swala la upotevu wa maji mnapaswa kujipanga ili mlishulikie maana kwa hapa Dodoma mjini inaonekana asilimia 30 bado kuna upotevu wa maji hivyo hakikisheni mnalifuatilia na kuliondoa kabisa maana maji yanayopotea bure huku kunawananchi hawapati kabisa maji naami hilo liko ndani ya uwezo wenu lishuulikieni kwa kulizibiti kabisa”alisisitiza Shekimweri.


Shekimweri amesema kuwa kwa utendaji mzuri alioufanya Meneja Ufundi wa duwasa Mhandisi Mayunga Kashilimu ndio matokeo mazuri ya kupandishwa cheo hivyo kwa wataalamu wengine wa duwasa mnatakiwa kuiga mfano wake wa utendaji wa kazi
“mayunga alikuwa mwadilifu,msikivu na mpole na hajikwazi amekuwa akifanya kazi usiku na mchana na ukimpigia simu kumweleza tatizo la maji anakusikiliza na kulifanyia kazi kwa wakati hivyo ndio vimemfanya amefanya kazi yake vizuri na sasa amepandishwa cheo sasa atakapo kuwa kwenye majukumu anatakiwa kuongeza juhudi zaidi ili kuhakikisha wananchi wanatatuliwa changamoto ya maji katika maeneo yao”alisisitiza Shekimweri.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »