TIGO NA BOA WARAHISISHA UWEKAJI WA AKIBA ‘Tigo Pesa kibubu’

TIGO NA BOA WARAHISISHA UWEKAJI WA AKIBA ‘Tigo Pesa kibubu’

Mtandao unaoongoza katika kuhakisha mtanzania anaishi maisha ya Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania na Benki ya Afrika(BOA)(Tanzania) wamezindua huduma mpya ya kuhifadhi pesa kwa kutumia simu ya mkononi ijulikanayo kama “TIGO PESA KIBUBU” itakayowawezesha wateja wa Tigo Pesa kutunza pesa zao na kupata gawio kupitia simu zao za mkononi. Tigo Pesa Kibubu ni huduma ya

Mtandao unaoongoza katika kuhakisha mtanzania anaishi maisha ya Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania na Benki ya Afrika(BOA)(Tanzania) wamezindua huduma mpya ya kuhifadhi pesa kwa kutumia simu ya mkononi ijulikanayo kama “TIGO PESA KIBUBU” itakayowawezesha wateja wa Tigo Pesa kutunza pesa zao na kupata gawio kupitia simu zao za mkononi.


Tigo Pesa Kibubu ni huduma ya kuhifadhi pesa itakayounganishwa kupitia akaunti kuu ya Tigo Pesa ambapo mtumiaji ataweza kuhifadhi pesa zake kidogokidogo kuanzia Tsh. 1 na kupata gawio pale atakapohifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadae.

Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha- Tigo Pesa,Angelica Pesha

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha- Tigo Pesa,Angelica Pesha amesema.
“Uzinduzi wa Tigo Pesa Kibubu umetokana na kuongezeka kwa idadi ya watanzania hasa ambao wanafanya miamala na kufanya huduma mbalimbali za kifedha kupitia Tigo Pesa ambapo kwasasa takwimu zinaonesha kuwa watumiaji wa Tigo Pesa wameongezeka hadi kufikia takriban Millioni 9 nchi nzima na sisi kama Tigo kwa kushirikiana na BOA kwa kuwajali wateja wetu tukaamua kuwaletea huduma hii ya TIGO PESA KIBUBU ili wafurahie kuhifadhi pesa zao kidigitali kwa ajili ya matumizi ya baadae huku wakipata gawio kulingana na kiasi cha Pesa watakachohifadhi” . Alisema Pesha.


“Huduma hii inaruhusu wateja wa Tigo Pesa kuhifadhi pesa na kupata gawio kulingana na salio liliopo. Gawio unaopatikana kila siku utakusanywa na kulipwa kila mwezi kulingana na salio ambalo litabaki kwenye mkoba wa mteja wa Tigo Pesa Kibubu. Mteja anaweza kutoa au kuokoa salio linalolingana wakati wowote. ” Alielezea Pesha.

“Ujumuishaji wa kifedha sio mwisho wenyewe. Kuendelea kutumika kwa huduma za kifedha na ubora wake. Ushirikiano wetu na BOA utaleta tabia mpya ya kuhifadhi fedha katika uchumi, ambapo wateja watahifadhi fedha kidijitali na kupata gawio. Kwa bidhaa hii mpya, tunawapa wateja wa Tigo Pesa njia bora ya kufikia malengo yao. Tunaamini ya kwamba, kiwango chao cha maisha kiuchumi, kitakuwa na mtazamo mzuri. ” Alisema Pesha.

Naibu Mkurugenzi mtendaji kutoka BOA, Wasia Mushi (Kulia)

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi mtendaji kutoka BOA, Wasia Mushi amesema kuwa
“Kama BOA tunajivunia kushirikiana na wenzetu wa Tigo katika kuwapelekea huduma mamilioni ya wananchi hasa ambao wako nje ya mfumo rasmi wa kibenki, Ni matumaini yetu kuwa huduma hii itarahisisha maisha na kukuza ujumuishaji wa kifedha, Benki kwa kushirikiana na Tigo tutakuwa msitari wa mbele kuhakikisha huduma hii inafanikiwa na kama shirika la kimataifa tunaamini kuwa ushirikiano huu wa TIGO na BOA utafungua njia ya kushirikiana zaidi ili kubuni na kuendelea kutoa huduma mbalimbali za kidigitali kwa watanzania” Alisema Mushi.


Huduma ya TIGO PESA KIBUBU itapatikana kwa kubonyeza MENU kuu ya Tigo Pesa ambayo ni 15001# lakini pia kupitia TIGO PESA APP.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »