Na Barnabas Kisengi, Dodoma WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamaii Jinsia Wazee na Watoto imetekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa aliyoyatoa Mkoani Katavi Agosti 27 Mwaka huu alipotembelea Hospitali ya Mkoa huo. Akizungumza na Waandishi wa Habari,hii leo Jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Profesa Abel Makubi kuhusiana na maagizo hayo amesema kuwa miongoni mwa
Na Barnabas Kisengi, Dodoma
WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamaii Jinsia Wazee na Watoto imetekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa aliyoyatoa Mkoani Katavi Agosti 27 Mwaka huu alipotembelea Hospitali ya Mkoa huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari,hii leo Jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Profesa Abel Makubi kuhusiana na maagizo hayo amesema kuwa miongoni mwa maagizo hayo ni pamoja na Wizara ya Afya kutakiwa irudishe usimamizi wa mradi wa ujenzi wa Hopsitali ya Mkoa huo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi.
Amesema maagizo mengine ni Katibu Tawala mkoa wa Katavi kutakiwa aunde kamati zitakazowezesha utekelezaji wa ujenzi wa jengo la Hospitali ya Mkoa pamoja na fedha za utekelezaji wa mradi kiasi cha sh Milioni 688 zihamishiwe kwa katibu tawala wa Mkoa wa Katavi.
Hata hivyo Profesa Makubi ameeleza kuwa katika kuhakikisha Hospitali hiyo inakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi bila kuchelewa,Wizara imeshaandaa mahitaji halisi ya vifaa,samani,TEHAMA na wataalam ,mchakato wa upatikanaji wa vifaa hivyo umeshaanza.
Pia amesema kutokana na umuhimu wa kuzishirikisha Ofsi za Wakuu wa Mikoa katika utekelezaji wa miradi hiyo kuna umuhimu kwa jamii kuanzia sasa kushiriki kikamilifu katika miradi hiyo.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *