DC WA MPWAPWA ALIPONGEZA JESHI LA POLISI WILAYANI HUMO

DC WA MPWAPWA ALIPONGEZA JESHI LA POLISI WILAYANI HUMO

Na Barnabas Kisengi, Mpwapwa  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Mwalimu Josephat Maganga amelipongeza Jeshi la Polisi wilayani Mpwapwa kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda amani na utulivu wilayani mpwapwa ambapo hivi karibuni kulitokea kikundi kilichokuwa kinawashambulia baadhi ya viongozi wa Kata na vijiji wilayani hapo. Pongezi hizo amezitoa katika kikao cha baraza la madiwani

Na Barnabas Kisengi, Mpwapwa 


Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Mwalimu Josephat Maganga amelipongeza Jeshi la Polisi wilayani Mpwapwa kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda amani na utulivu wilayani mpwapwa ambapo hivi karibuni kulitokea kikundi kilichokuwa kinawashambulia baadhi ya viongozi wa Kata na vijiji wilayani hapo. 
Pongezi hizo amezitoa katika kikao cha baraza la madiwani wilayani hapo wakati akitoa taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambayo yeye ndio mwenyekiti wa kamati hiyo. 

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mwalimu Josephat Maganga


“Napenda kulipongeza Jeshi la police kwa kazi mnazofanya  za kulinda amani na utulivu wilayani hapa na kipekee nikupongeze Mkuu wa Police wa wilaya (OCD) afande COSMAS MBOYA kwa kazi nzuri unayoifanya katika kuwalinda wananchi na mali zao na kuifanya mpwapwa kuwa na utulivu na amani hadi sasa”amesema Mkuu wa wilaya


Aidha Mkuu wa wilaya hiyo Mwalimu JOSEPHT MAGANGA amesema hivi karibuni kuna watu walikuwa wakiwavamia viongozi wa Kata na vijiji lalini waliweza kuzibitiwa na Jeshi hilo na sasa mpwapwa iko shwari kwakuwa OCD MBOYA ametimiza wajibu wake na pia mjue Jeshi la police liko imara kushulika na wahalifu. 
“hata hivyo nyinyi madiwani leo hapa tumpongeze Mkuu wa Police wilaya OCD MBOYA kwa kazi nzuri anayoifanya kuhakikisha wilaya iko salama Mimi Kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ninafarijika ninapo ona wilaya yangu ninayoiongoza iko salama na nimezunguka katika Kata na vijiji na vitongoji nimefurahi kukuta Kuna vikundi vya ulinzi shirikishi na police Kata wapo katika maeneo yao hapo OCD MBOYA nirudie tena kukupongeza sana kwa kazi nzuri ya kulinda amani pia pongezi hizo ziwafikie na askari wako wote wa wilaya kwa kazi nzuri ya kuhakikisha mpwapwa iko salama endeleeni kupiga kazi kwa uadilifu na uzalendo uliotukuka”alisisitiza Maganga.


Aidha Mwalimu Maganga amewataka waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanashirikiana na police Kata na vikundi vya ulinzi shirikishi kuhakikisha wanakuwa wanasima vizuri hali ya ulinzi na usalama katika Kata,vijiji na vitongoji katika maeneo wanayotoka ili wilaya iendelee kuwa shwari.

Mkuu wa Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD  COSMAS MBOYA


Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD  COSMAS MBOYA  amemshukuru Mkuu wa wilaya na Baraza la madiwani kwa kumpa pongezi zake binafsi na kwa police wote wa wilaya ya mpwapwa na amesema kulinda watu na mali zao na kuhakikisha wilaya iko salama ni wajibu wao Kama police ni lazima wawajibike kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama vinaendelea kuwepo wilayani hapo. 
“Pia niendelee kuwasisitiza waheshimiwa Madiwani tuendelee kushirikiana na police Kata katika Kata zenu na kutujulisha pindi kunakokuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani au wizi basi mnakuwa mnatujulisha ili tuweze kuchukua hatua pindi dalili hizo mkiziona kwakuwa Sisi tunafanya kazi masaa 24 siku zote na muda wote tuko kazini hapo wilaya yetu itaendelea kuwa salama muda wote”amesema OCD Mboya

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »