AFISA MAZINGIRA MPWAPWA ATAKIWA KUCHUKUA HATUA ZA KISHERIA KWA WANAOHARIBU MAZINGIRA

AFISA MAZINGIRA MPWAPWA ATAKIWA KUCHUKUA HATUA ZA KISHERIA KWA WANAOHARIBU MAZINGIRA

Na Barnabas Kisengi, Mpwapwa  Kamati ya kudumu ya uchumi, ujenzi na mazingira ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imemwagiza Afisa mazingira wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanatumia sheria ndogo ndogo za Halimashauri kuhakikisha wanawachukulia hatuo watu wanaoharibu mazingira wilayani hapo.  Akitoa taarifa ya kamati hiyo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa

Na Barnabas Kisengi, Mpwapwa 


Kamati ya kudumu ya uchumi, ujenzi na mazingira ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imemwagiza Afisa mazingira wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanatumia sheria ndogo ndogo za Halimashauri kuhakikisha wanawachukulia hatuo watu wanaoharibu mazingira wilayani hapo. 


Akitoa taarifa ya kamati hiyo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya uchumi, ujenzi na mazingira  Diwani wa Kata ya Pwaga Jimbo la Kibakwe Mhe.Willfred Mgonela amesema bado kunabaadhi ya maeneo wilayani hapo yanauharibifu wa mazingira jambo ambalo hupelekea maeneo mengi kuharibika na kuwa na makorongo mengi. 


Mgonela amesema kamati imemwagiza Afisa mazingira wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanatumia sheria ndogondogo zilizo tungwa kwa kuwachukulia wananchi hatua kwa wale wanaona haribu mazingira wilayani hapo. 


Aidha kamati imezitaka kamati za mazingira katika Kata,vijiji na vitongoji kuhakikisha zinawajibika ipasavyo kushulika na watu wenyetabia ya kuharibu mazingira wilayani hapo
“kumekuwa kuna kamati za mazingira katika vijiji na vitongoji zimejisahau kutekeleza wajibu wao wa kulinda mazingira katika maeneo yao maana kuna vijiji ukipita unakuta kuna uharibifu wa mazingira sasa tunashangaa hizo kamati zinakuwa wapi hadi watu wanachoma mikaa milimani wanalima kwenye vyanzo vya maji na kwenye makorongo”amsema Mgonela.


Mgonela amesema kupitia afisa mazingira wa halmashauri sasa apite  kwenye Kata zote 33 za Wilaya ya Mpwapwa aangalie na kufanya tathumini ya hali ya uharibifu wa mazingira na kuwaletea taarifa kwenye kamati hiyo na pia azikumbushe kamati za mazingira za Kata, vijiji na vitongoji majukumu yao ili waweze kuendelea kulinda mazingira katika maeneo yao. 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »