TIGO NA INFINIX WAJA NA SIMU MPYA ” Infinix ZERO X PRO”

TIGO NA INFINIX WAJA NA SIMU MPYA ”  Infinix ZERO X PRO”

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania imeshirikiana na Infinix Tanzania kuzindua simu janja toleo jipya yenye kiwango cha juu ya 108MP na 60x kamera, ijulikanayo kama Infinix ZERO X PRO, ambayo itauzwa kuanzia 800,000 Tsh. Akizungumza wakati wa kutangaza simu hiyo Mkuu wa Kitengo cha maduka na Bidhaa za

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania imeshirikiana na Infinix Tanzania kuzindua simu janja toleo jipya yenye kiwango cha juu ya 108MP na 60x kamera, ijulikanayo kama Infinix ZERO X PRO, ambayo itauzwa kuanzia 800,000 Tsh.

Akizungumza wakati wa kutangaza simu hiyo Mkuu wa Kitengo cha maduka na Bidhaa za Intaneti Tigo Tanzania Bwana Mkumbo Myonga amesema kuwa

 “Ushirikiano wa Tigo na Infinix Tanzania unaonyesha zaidi lengo la kuunganisha nguvu na kuwa Vinara katika utoaji wa huduma za Kidigitali nchini Tanzania, kwa kuongeza upatikanaji wa simu bora sokoni zitakazochochea kuongezeka kwa huduma za Kidigitali.

Myonga pia ameongeza kuwa, “kuzindua Infinix Zero X PRO kunadhiirisha kwamba wateja wa Tigo watajipatia kilicho bora, suala litakalochangia kuongeza thamani ya mazingira ya kibiashara nchini.”

Kulingana na Myonga “Simu hizo zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini kote na zitakua na Ofa ya GB 96 za Intaneti Bure kutumia mwaka mzima. “

Kwa Upande Mwingine, Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa, alisema kuwa “kutangazwa kwa toleo jipya la simu ya Infinix zero x pro kunadhiirisha maana halisi ya teknolojia maana teknolojia inahusisha Uvumbuzi wa bidhaa mpya na kuvuka mipaka zaidi na zaidi ili kuwafikia wateja kiurahisi na Infinix ZERO X pro inamwezesha mtumiaji kufanya vitu vingi kwa pamoja maana ina processor ya Helio G95 kwa ajili ya  kucheza GAME n.k, ”

Bi Aisha pia ameongeza “Infinix zero x inakuja na Skrini ya 6.67FHD + AMOLED na 120hz na yenye kuonyesha picha nzuri na yenye ubora wa juu lensi 60x  inayotoa picha nzuri hata kama ni usiku, na kamera kuu ya 108MP IOS.

Infinix ZERO X pro sasa inapatikana katika maduka ya Infinix na Tigo nchi nzima .

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »