TIGO KILI HALF MARATHON 2022 YAZINDULIWA RASMI

TIGO KILI HALF MARATHON 2022 YAZINDULIWA RASMI

Na Mwandishi Wetu Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania kwa mara ya saba mfululizo imeendelea kudhamini Mashindano ya Mbio za Riadha Kilomita 21 maarufu kama TIGO KILI HALF MARATHON , ambayo Uzinduzi wake kwa Mwaka 2022 umefanyika Oktoba 13, 2021 Jijini Dar Es Salaam Akizungumza katika Uzinduzi huo Mwakilishi

Na Mwandishi Wetu

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania kwa mara ya saba mfululizo imeendelea kudhamini Mashindano ya Mbio za Riadha Kilomita 21 maarufu kama TIGO KILI HALF MARATHON , ambayo Uzinduzi wake kwa Mwaka 2022 umefanyika Oktoba 13, 2021 Jijini Dar Es Salaam

Mwakilishi kutoka Kampuni ya Tigo Tanzania Bi. Anna Loya

Akizungumza katika Uzinduzi huo Mwakilishi kutoka Kampuni ya Tigo Tanzania Bi. Anna Loya amewapongeza waandaaji wa Kilimanjaro Marathon kwa Kufikisha miaka 20 ya Kuandaa , kuratibu mbio hizi za kimataifa.

“Mwaka huu, Tigo imedhamini tena mbio hizi maarufu za Tigo Kili Half Marathon (Km 21) ikiwa ni mara ya saba mfululizo, ili kutoa fursa kwa watanzania na watu kutoka nchi jirani kushiriki, kubadilishana tamaduni,kuburudika na kufurahi kwa pamoja.
Pia Mwaka huu tulizindua mradi wetu wa Tigo Green for Kili wenye na dhamira ya kuboresha mazingira na kurudisha theluji katika Mlima Kilimanjaro, Mradii huu endelevu ulikua na engo la kupanda miche 28,000 lakini kwa muamko wa wananchi na wadau hadi mwisho wa mwaka huu utaoanda miche 31,000. Zoezi hili litaendelea mwakani na tutatoa taarifa zaidi tutakapozindua rasmi Tigo half Marahon mwezi wa kwanza , 2022 mjini Moshi.

Pia Tunawakumbusha watanzania wote ambao wangependa kushiriki kwenye mbio hizi, kujisajili mapema ili waweze kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki.


Dirisha la usajili kwaajili ya Tigo Kili Half Marathon pamoja na mbio za Km 42 na Km5 limekwisha kufunguliwa na wateja wa Tigo wanaweza kupiga 14920# ili kujisajili, kuchagua aina ya mbio anazotaka kushiriki na kufanya malipo. Baadaye atapokea ujumbe wa kuthibitisha malipo yake.
Mshiriki wa mbio hizi anatakiwa kuhifadhi ujumbe (SMS) na atatumia kama uthibitisho akiambatanisha na kitambulisho chake wakati wa kuchukua namba ya ushiriki katika vituo vilivyopo Dar es Salaam, Arusha na Moshi.


Katika mbio hizi, Tigo inatoa zawadi za fedha zenye thamani ya Shilingi Milioni 12 kwa washindi 10 wa kwanza wa Kili Half Marathon. Pia,washiriki 4,500 watakaomaliza Km 21 watapewa medali za heshima.Vilevile, tutatoa vyeti kwa washiriki wote wa Kili Half Marathon.


Mwisho kabisa Tungependa kuwakumbusha wateja wetu kua wataweza kuwatumia marafiki, ndugu na jamaa, matukio yatakayokuwa yanaendelea siku ya Tigo Kili Half Marathon o kupitia mtandao wetu ulioboreshwa wa Tigo 4G+.” Alimalizia Bi. Anna

Mhe. Jaji Thomas Mihayo.

Ikumbukwe kuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo alikua Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye aliwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Mhe. Jaji Thomas Mihayo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »