Rais Dkt. Mwinyi, amesema tukio la kuwakumbuka viongozi wa Tanzania waliotangulia mbele ya haki ni muhimu sana.

Rais Dkt. Mwinyi, amesema tukio la kuwakumbuka viongozi wa Tanzania waliotangulia mbele ya haki ni muhimu sana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema tukio la kuwakumbuka viongozi wa Tanzania waliotangulia mbele ya haki ni muhimu sana kwa sababu muda wote walijitoa muhanga kwa nchi yao na kujenga taifa lililo huru lenye kuzingatia haki na usawa bila ya kujali rangi,kabila wala dini. Rais Dk.Mwinyi aliyaeleza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema tukio la kuwakumbuka viongozi wa Tanzania waliotangulia mbele ya haki ni muhimu sana kwa sababu muda wote walijitoa muhanga kwa nchi yao na kujenga taifa lililo huru lenye kuzingatia haki na usawa bila ya kujali rangi,kabila wala dini.

Rais Dk.Mwinyi aliyaeleza hayo aliposhiriki Misa na Ibada Maalumu yenye lengo la kuwaombea viongozi mbalimbali waliokwisha tangulia  mbele ya haki katika Kanisa Katoliki Mtakatifu Bikira Maria Mkoani Geita Wilaya ya Chato.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi alisema Uhuru,fursa na maendeleo zinazoendelea kushuhudiwa hadi hii leo ni matunda na jasho ya hekma zao   hivyo ni wajibu kuziendeleza na kuwarithisha kizazi kijacho.

Rais Dk.Hussein Mwinyi ambae aliambatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi amemshukuru Mhashamu Baba Askofu Severine na Maaskofu wengine na waumini wa dini mbalimbali nchini kwa kufanikisha vyema sala na maombi kwa ajili ya viongozi wakuu waliokwisha tangulia mbele ya haki na kuwataka wananchi kuendelea kuienzi na kuiendeleza Amani iliyopo nchini kwani ni Tunu kwa Taifa la Tanzania.

Mapema Baba Askofu Mhasham Severine Niwemgizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Ngara ambae ndie alieongoza Ibada hio ya kuwaombea viongozi wa Tanzania waliokwisha tangulia mbele ya Haki amemshukuru Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa Kuwapa heshima na kujumuika nao katika Ibada hio.

Vile vile amewaasa viongozi,waumini na wananchi waliohudhuria katika Ibada hio Kumtanguliza Mungu Mbele katika maisha yao na kuwaeleza kuwa hata viongozi ambao wanaowakumbuka katika Ibada hio walidhihirisha.

Ibada hio ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,ni kwa ajili ya kuwaombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,Hayati Abeid Amani Karume Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Benjamin Willium Mkapa na Merehemu John Pombe Magufuli.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »