Wizara ya Afya imewataka wadau wa Afya kutoa elimu na kuhamasisha mabadiliko ya tabia kuhusu unawaji mikono.

Wizara ya Afya imewataka wadau wa Afya kutoa elimu na kuhamasisha mabadiliko ya tabia kuhusu unawaji mikono.

IKIWA leo Dunia inaadhimisha siku ya kunawa mikono  Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetoa wito kwa wadau wote wa masuala ya afya mazingira na usafi kote nchini, kushirikiana na serikali katika kutoa elimu na kuhamasisha mabadiliko  ya tabia  kuhusu unawaji mikono. Wito huo umetolewa hii leo Jijini Dodoma  na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga

IKIWA leo Dunia inaadhimisha siku ya kunawa mikono  Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetoa wito kwa wadau wote wa masuala ya afya mazingira na usafi kote nchini, kushirikiana na serikali katika kutoa elimu na kuhamasisha mabadiliko  ya tabia  kuhusu unawaji mikono.

Wito huo umetolewa hii leo Jijini Dodoma  na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga Dkt Ahmed Makuani wakati akitoa tamko kwa niaba ya Waziri wa Afya Dkt Dorothy Gwajima kuhusu maadhimisho ya siku ya kunawa mikono Duniani yanayoadhimishwa Oktoba 15 ya kila mwaka.

Dkt Makuani, amesema usafi wa mikono ni miongoni mwa njia muhimu zinazosaidia sana kujilinda na kuzuia kuenea kwa magonjwa ya homa kali ya mapafu (UVIKO-19), hivyo Wizara imeendelea kukumbusha suala la usafi wa mikono kila mwaka kutokana na umuhimu wake Katika kuzuia na kukinga maambukizi ya magonjwa kama vile kipindupindu, Ebola , kuhara damu ,minyoo, magonjwa ya macho pamoja na maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa hewa ya mapafu ambayo kwa kiasi kikubwa yanaweza kuepukika kwa  kunawa mikono.

Aidha  amebainisha kuwa kwa mujibu Shirika la Afya Duniani WHO  pamoja na UNICEF zinaonesha kuwa asilimia 60% ya watu Duniani sawa na watatu  (3) kati ya watano (5) hunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.

Hatahivyo, amesema hapa nchini kaya zenye vifaa vya kunawa kwa maji na sabuni zimeongezeka kutoka 21% mwaka 2019 hadi 41.8% mwezi juni 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »