Mkurugenzi Siajabu Pandu amewataka washiriki wa Miradi ya ajira za muda kuyatumia vyema Mafunzo waliyoyapata .

Mkurugenzi Siajabu Pandu amewataka washiriki wa Miradi ya ajira za muda kuyatumia vyema Mafunzo waliyoyapata .

Mkurugenzi Idara ya Uratibu Shughuli za Serikali Ndugu Siajabu Sleiman Pandu amewataka washiriki wa Miradi ya ajira za muda kuyatumia vyema Mafunzo waliyoyapata ili kufanikisha lengo lililokusudiwa. Mkurugenzi Sijaabu amesema hayo  katika Ukumbi wa Betres Nkurumah wakati wa akiyafunga rasmi Mafunzo ya siku tatu yaliyowashirikisha wawezeshaji kutoka shehia mbali mbali za Unguja ambapo amewataka kuwa

Mkurugenzi Idara ya Uratibu Shughuli za Serikali Ndugu Siajabu Sleiman Pandu amewataka washiriki wa Miradi ya ajira za muda kuyatumia vyema Mafunzo waliyoyapata ili kufanikisha lengo lililokusudiwa.

Mkurugenzi Sijaabu amesema hayo  katika Ukumbi wa Betres Nkurumah wakati wa akiyafunga rasmi Mafunzo ya siku tatu yaliyowashirikisha wawezeshaji kutoka shehia mbali mbali za Unguja ambapo amewataka kuwa makini kwa kutoa taarifa sahihi za Walengwa kutokana na umuhimu wake katika kufanikisha mipango ya serikali.

Amesema taarifa hizo zitasaidia kupunguza malalamiko kwa Walengwa watakaoibuliwa katika kutekeleza ajira za muda katika Sheiha zao.

Nae, Mratibu wa Tasaf Zanzibar Saida Salehe amewataka washiriki hao  kufanye kazi  kwa kuzingatia taratibu  zilizowekwa kwani Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar  inatarajia matokeo yatakayo leta tija katika utekelezaji wa Miradi hiyo

Nao washiriki wa Mafunzo  hayo wameushukuru uwongozi wa Ofisi ya Makamu wa Pili  wa Rais kwa kuwaandalia Mafunzo hayo na kuahidi  kuyafanyia kazi  mafunzo kama inavo tarajiwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »