WAZIRI NDUMBARO ATOA WITO KWA WATOA HUDUMA ZA WATALII NCHINI KUWA MSTARI WA MBELE KUCHANJA ILI KUJIKINGA NA UVIKO 19

WAZIRI NDUMBARO ATOA  WITO KWA WATOA HUDUMA ZA WATALII NCHINI KUWA MSTARI WA MBELE KUCHANJA ILI KUJIKINGA NA UVIKO 19

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ametoa wito kwa Watoa huduma za Watalii kuwa mstari wa mbele kuchanja ili kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya  UVIKO 19Pia,Dkt.Ndumbaro amesema kitendo cha  Watoa huduma wengi  katika sekta ya utalii kuchanja ni jambo la  muhimu  kwani watalii wanaokuja nchini wanapata ujasiri  kuwa nchi wanayotembelea ni salama na

Waziri wa  wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa nne kulia)  akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Watalii ( TATO) , Willy Chamburo  mara baada ya kukabidhi  mfano wa hundi ya kiasi cha Shilingi milioni 150 kwa Waziri huyo ikiwa ni pesa ambayo ni  makusanyo yaliyofanywa na TATO  kwenye vituo vya kutolea sampuli kwa ajili ya vipimo vya corona kwa wageni katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kipindi cha mwaka jana, hafla hiyo ya kukabidhi hundi imefanyika jana Jijini Arusha huku ikishuhudiwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer ( wa kwanza kulia)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa nne kulia) akizungumza  na Wadau wa utalii pamoja na Wataalam mbalimbali walioshiriki katila mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya        (European Business Group) kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utalii nchini ambapo ameahidu kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( kushoto) akiwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer (  kulia) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utalii nchini katika mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya        (European Business Group) 
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer akizungumza  na Wadau wa utalii pamoja na Wataalam mbalimbali walioshiriki katila mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya        (European Business Group) kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utalii nchini 
Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya        (European Business Group), Cikay Richards  akizungumza na Washiriki wa mkutano wa kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini kabla ya mkutano huo kuanza 
6.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa nne kulia ) Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer ( katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu wa masuala ya utangazaji utalii pamoja na Wadau wa Utalii nchini mara baada ya kumaliza  mkutano huo.
7.Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya        (European Business Group) kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utalii nchini 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ametoa wito kwa Watoa huduma za Watalii kuwa mstari wa mbele kuchanja ili kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya  UVIKO 19
Pia,Dkt.Ndumbaro amesema kitendo cha  Watoa huduma wengi  katika sekta ya utalii kuchanja ni jambo la  muhimu  kwani watalii wanaokuja nchini wanapata ujasiri  kuwa nchi wanayotembelea ni salama na hivyo  hawawezi kupata maambukizi 

Ametoa wito huo leo Jijini Arusha  wakati alipokuwa  akizungumza  kwenye  mkutano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya ( European Business Group) uliowakutanisha Wadau mbalimbali wa Utalii nchini kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili sekta ya utalii nchini
Katika mkutano uliwaokutanisha wataalamu mbalimbali  kwa upande wa Serikali uliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro huku kwa upande Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Ulaya uliongozwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wiebe de Boer

Dkt.Ndumbaro amefafanua kuwa  watalii waingiapo nchini huhitaji huduma kama vile malazi, chakula uongozwaji, starehe kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii pamoja na kununua bidhaa mbalimbali za kiutamaduni kwa ajili ya matumizi yao na kubeba kama zawadi, ni muhimu watu wa sehemu hizi kuchanja ili kujilinda 
Ameongoza kuwa  Watu wote wanaotoa huduma katika maeneo hayo  wanawajibika kuwa mstari wa mbele kuchanja ili kuendelea na shughuli za utalii bila kuhatarisha  afya na maisha  yao na  wanaowapa huduma .

” Wanatoa huduma ambao hawajachanjwa wapo hatarini  zaidi kupoteza maisha yao kwa vile wanakutana na watu wa kutoka mataifa mbalimbali duniani hususani yale ambayo yana maambukizi makubwa ya UVIKO 19, Nawasihi kwa usalama wa maisha yao wachanje” amesisitiza Dkt.Ndumbaro 
” Lazima mtambue kuwa watalii wengi hutokea  nchi za Ulaya, Amerika na Asia ambazo hadi wakati huu bado zina viwango vya juu vya maambukizi ya UVIKO 19” alisisitiza Dkt. Ndumbaro

Amesema tangu  Serikali ya Tanzania iliporidhia kupokea chanjo watalii wameanza kumiminika kuja nchini kwa vile wanaujasiri kwa kuamini kuwa sehemu wanayokwenda ni salama kwa ajili ya afya zao, tunamshukuru sana 
Hata hivyo , Dkt.Ndumbaro amewataka watoa huduma kwa watalii wale waliochanja na wale ambao bado kuendelea kuzingatia  taratibu zilizowekwa na Wizara hiyo pindi wanapowahudumia watalii kuhakikisha wqnachukua tahadhari zote ikiwemo kuvaswanavaa barakoa muda wote.
Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amesema Wizara anayoiongoza imeshaanza mazungumzo na Wizara ya Afya, Jinsia na Watoto kuona uwezekano wa kuwaruhusu watalii wanaokuja nchini ambao wamepimwa ndani ya masas 72 na waliochanjwa kutokupima tena pindi wanapowasili katika viwanja vya ndege na mipakani.
Kwa upande wake Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe.Wieber de Boer amesema Serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa namba moja katika kutoa ajira nchini ikiwemo kutoa mafunzo pamoja na kujenga miundombinu kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu sekta ya utalii kama ilivyosaidia kujenga Chuo cha Taifa cha Utalii pamoja na kuandaa miongozo ya kutangaza sekta ya utalii inayotumika nchini
” Uholanzi ni Wadau wakubwa wa maendeleo katika nchi hii hususani katika masuala ya utalii tunaiahidi Serikali kuendelea kushirikiana kwa namna yoyote ile hasa katika nyakati ambazo sekta ya utalii imeshambuliwa na UVIKO 19” alisisitiza Mhe. Balozi Boer

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »