ZIARA YA MAKATIBU WAKUU KASULU MKOANI KIGOMA

ZIARA YA MAKATIBU WAKUU KASULU MKOANI KIGOMA

Na Mwandishi wetu, Kasulu Watanzania wamemeadharishwa dhidi ya madhara ya yanayoweza kutokana na tabia ya kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na wasitegemee msaada zaidi kutoka nyumba salama kwa ajili ya  kuwarejesha wahanga wa ukatili katika hali ya awali. Taadhari hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya Idara Kuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akitambulisha nia ya Ziara ya Makatibu Wakuu Watatu katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Mwakisu walipowasili Ofisini kwake, Wilayani Kasulu, Kigoma. 
2Makatibu Wakuu, Prof. Sifuni Mchome(Katiba na Sheria), Dkt. John Jingu(Afya, Maendeleo ya Jamii) na Christopher Kadio(Mambo ya Ndani ya Nchi wakipata Maelezo juu ya Uendeshaji wa Nyumba Salama ya Wote Sawa iliyoko Kasulu, Mkoani Kigoma. 
Makatibu Wakuu, Prof. Sifuni Mchome(Katiba na Sheria), Dkt. John Jingu(Afya, Maendeleo ya Jamii) na Christopher Kadio(Mambo ya Ndani ya Nchi) katika picha ya pamoja na wataalam na wafanyakazi wa nyumba salama ya wote sawa iliyoko Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma

Na Mwandishi wetu, Kasulu

Watanzania wamemeadharishwa dhidi ya madhara ya yanayoweza kutokana na tabia ya kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na wasitegemee msaada zaidi kutoka nyumba salama kwa ajili ya  kuwarejesha wahanga wa ukatili katika hali ya awali.

Taadhari hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu mjini Kasulu katika kikao kazi na Makatibu Wakuu, Profesa Sifuni Mchome wa Katiba na Sheria na Christopher Kadio wa Mambo ya Ndani ya Nchi walipofanya ziara katika Nyumba Salama kwa ajili ya hifadhi ya muda kwa wahanga wa ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Dkt. Jingu amesema nyumba salama zimeanzishwa baada ya jamii kushindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda maadili mila na desturi ambazo zingesaidia katika malezi na makuzi ya watoto na kujenga kizazi cha imara kisichokabiliwa na vitendo vya uhalifu.

 “Nyumba salama ni jambo muhimu katika kulinda haki na ustawi wa aliyefanyiwa ukatili, lakini ni jambo ambalo lisingepaswa kama kila mmoja angekuwa anatimiza jukumu lake….jambo la usalama na ulinzi na malezi ni kazi ya jamii , Tusiaachie serikali wala polisi kulinda haki za makundi haya, bali wote kama jamii  Wote kama jamii tupambane na kuwakemea wote wananofanya vitendo vya ukatili vinginevyo ,  tutaharibikiwa.

 Jamii itimize jukumu lake kwa kushirikiana na serikali kwa kuwa inajua nani anahusika kwa namna gani. Alisisitiza.Aliongeza na kuishauri jamii kuhakikisha kwamba inashiriki kikamilifu kuwafichua wale wote wanaokwamisha maendeleo ya jamii ili Amani iweze kutawala miongoni mwa wanajamii.Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome amewataka kamati za ulinzi wan a usalama wa wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya ukatili zifanye kazi kazi kama ilivyoelekezwa ili kuondokana na kadhia hiyo.
Profesa Mchome amesema tayari mhimili wa mahakama umetoa mwongozo wa kushughulikia kesi zinazowahusu watoto ndani ya muda mfupi ili haki iweze kuchukua mkondo wake.

Akizungumzia utekelezaji wa Mpango wa kutokomeza vitendo vya Ukatili kwa wanawake na watoto, Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio amesema vyombo vilivyo chini ya Wizara yake vitaendeleza jitihada za kukomesha ukatili wa aina yoyote. 

Akitoa ripoti mbele ya Makatibu Wakuu watatu, Meneja wa nyumba salama ya wote sawa ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wanaolenga kukabiliana na vitendo vya ukatili katika jamii.Makatibu Wakuu watatu, wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Katiba na Sheria na Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wako katika ziara ya pamoja kwa lengo la kufuatilia shughuli mbalimbali za maendeleo, kuainisha changamoto na kutafuta suluhisho la pamoja na kwa haraka. mwisho

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »