RAIS MWINYI AMEFUNGA MAFUNZO YA POLISI SAJIN (SGT)MTERA MOROGORO

RAIS MWINYI AMEFUNGA MAFUNZO YA POLISI SAJIN (SGT)MTERA MOROGORO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 16 Oktoba, 2021 amewatunuku vyeti na kuwapandisha vyeo Askari wahitimu mia saba kumi na sita (716) wa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 16 Oktoba, 2021 amewatunuku vyeti na kuwapandisha vyeo Askari wahitimu mia saba kumi na sita (716) wa mafunzo ya Uongozi ngazi ya Sajini(SGT).

Rais Dk. Mwinyi amewataka askari hao waliohitimu mafunzo yao kwenda kufanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi ya uaskari ikiwa ni pamoja na udhibiti wa siri na uadilifu.

“Jiepusheni na vishawishi mbalimbali vinavyoweza kulitia doa Jeshi la Polisi na Nchi yetu. Askari ni Kioo cha Jamii, Kwa hivyo mkiwa kazini na ndani ya jamii askari polisi awe ni mfano wa tabia njema na kutii sharia za nchi” Amesema Rais Dk. Mwinyi.

Aidha, Mhe. Rais ameongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo watendaji ili wakatekeleze majukumu yao ipasavyo katika kuilinda nchi na mipaka yake pamoja na kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii katika hali ya usalama na utulivu.

Mapema kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi,Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mheshimiwa George Boniface Simbachawene akataja Idadi ya wahitimu wa mafunzo hayo kwa vyuo vyote vya Polisi vilivyopo nchini.

akizungumza kwa niaba ya Inspekta Jeneral wa Polisi nchini Kamishna wa Polisi wa Utawala na Menejmenti ya rasilimali watu Benedict Wakuliyamba  akaeleza mwelekeo wa Jeshi la Polisi

Mahafali ya mafunzo hayo yamefanyika katika Chuo cha Maafisa Polisi Kidatu, Mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawe, Kamishna wa Polisi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu CP Benedict Wakuliyamba, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martin Shigela, Mkuu wa Chuo cha Maafisa Polisi Kidatu, ACP Zarau Mpangule pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »