WANAFUNZI 37,731 WAPANGIWA MIKOPO NA HESLB AWAMU YA KWANZA

WANAFUNZI 37,731 WAPANGIWA MIKOPO NA HESLB AWAMU YA KWANZA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza leo Oktoba 17, 2021 orodha ya Awamu ya Kwanza yenye wanafunzi 37,731 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya Tsh.Bilioni 99.9 kwa mwaka wa masomo 2021/2022 unaotarajiwa kuanzia wiki ijayo. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru ambapo amesema kuwa

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza leo Oktoba 17, 2021 orodha ya Awamu ya Kwanza yenye wanafunzi 37,731 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo yenye thamani ya Tsh.Bilioni 99.9 kwa mwaka wa masomo 2021/2022 unaotarajiwa kuanzia wiki ijayo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru ambapo amesema kuwa kati ya wanafunzi hao (37,731), wanaume ni 23,379 sawa na asilimia 62 na wanawake ni 14,352 sawa na asilimia 38.

Badru ameongeza kuwa HESLB imeanza kupeleka fedha za wanafunzi waliopangiwa mikopo katika vyuo mbalimbali na kuwataka wanafunzi kupata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mkopo maarufu kama SIPA (Student’s Individual Permanent Account) na kujiandaa kwenda vyuoni kwa ajili ya kujisajili.

“Serikali imeshatupatia fedha na tumeanza kuzipeleka vyuoni, lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wanaopangiwa wanazikuta fedha vyuoni ambako watajisajili na kupokea ili watimize ndoto zao” amesema Badru.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »