RC Makala ameongeza siku 12 machinga kuhama katika maeneo yaliyokatazwa.

RC Makala ameongeza siku 12 machinga kuhama katika maeneo yaliyokatazwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mhe. Amos Makalla ameongeza muda wa siku 12 kwa Wanaofanya biashara Kwenye maeneo yaliyokatazwa kuhama na kuwataka Wafanyabiashara kutumia muda huo kuhamia kwenye maeneo yaliyotengwa.RC Makalla ameongeza siku hizo Ili kutoa nafasi ya kutosha kwa Machinga hao kuhama ambapo amesema muda alioongeza ukimalizika asionekane Mfanyabiashara yoyote kwenye maeneo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mhe. Amos Makalla.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mhe. Amos Makalla ameongeza muda wa siku 12 kwa Wanaofanya biashara Kwenye maeneo yaliyokatazwa kuhama na kuwataka Wafanyabiashara kutumia muda huo kuhamia kwenye maeneo yaliyotengwa.
RC Makalla ameongeza siku hizo Ili kutoa nafasi ya kutosha kwa Machinga hao kuhama ambapo amesema muda alioongeza ukimalizika asionekane Mfanyabiashara yoyote kwenye maeneo yaliyokatazwa.
Akizungumza na Wafanyabiashara Kariakoo, RC Makalla ameelekeza eneo la DDC liboreshwe ili liweze kupokea Wafanyabiashara wengi zaidi tofauti na Sasa ambapo linatumika kuuza vyakula na Vinywaji.
Aidha RC Makalla amefurahishwa na mwitikio mzuri wa Wafanyabiashara kuhamia kwenye maeneo yaliyotengwa na kutoa wito kwa wengine kutumia muda uliotolewa kuhama.
Hata hivyo RC Makalla ameyataja makundi ya Wafanyabiashara wanaotakiwa kuhama ni pamoja na Wanaofanya biashara Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu, Wanaofanya biashara Kwenye hifadhi ya Barabara, Wanaofanya biashara mbele ya Maduka, Wanaofanya biashara Kwenye maeneo ya Umma na waliojenga Vibanda juu ya Mitaro na mifereji.
Miongoni mwa sababu zinazofanya Serikali kuamua kuwapanga vizuri Machinga ni kupotea kwa mandhari ya Jiji Kutokana na Uchafu, Ongezeko la ajali na foleni, Sababu za kiusalama Kutokana na Vibanda vilivyojengwa kutumika kuhifadhi wahalifu nyakati za usiku na upotevu wa Mapato ya Serikali Kutokana na Wafanyabiashara wakubwa kuwatumia Machinga kukwepa kodi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »