NAIBU WAZIRI SILINDE ATOA ONYO KWA WATUMISHI TSC

NAIBU WAZIRI SILINDE ATOA ONYO KWA WATUMISHI TSC

NAIBU  Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulikia Elimu,David Silinde,amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita haitasita kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya watendaji wa Tume ya watumishi ya Walimu Nchini [TSC] watakaobainika kujihusiha na  vitendo vya  rushwa. Silinde ametoa kauli hiyo hii leo Jijini Dodoma wakati akizindua kikao Kazi

NAIBU  Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulikia Elimu,David Silinde,amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita haitasita kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya watendaji wa Tume ya watumishi ya Walimu Nchini [TSC] watakaobainika kujihusiha na  vitendo vya  rushwa.

Silinde ametoa kauli hiyo hii leo Jijini Dodoma wakati akizindua kikao Kazi cha Makaimu Makatibu wasaidizi wa Tume ya Watumishi ya Walimu  kutoka wilaya139 nchini chenye lengo la kujitahmini kuhusu majukumu ya Tume hiyo.

Aidha  amewataka Makaimu Makatibu hao kusimamia vyema suala la maadili kwa walimu  ikiwa ni pamoja na kutenda haki kwani zaidi ya asilimia 60 ya watumishi wa umma ni walimu hivyo ana imani nao katika kutekeleza majukumu yao.

Sanjari na hilo,Naibu Waziri huyo ameziagiza Halmashauri ambazo hazijawapatia ofisi Makatibu hao kuwapatia mara moja kwani kinyume na hapo atawachukulia hatua huku akiwata watumishi wa Tume hiyo kusimamaia fedha  kiasi cha Shilingi bilioni 536 zilizotolewa na Rais kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa  kwani zinaenda kutekelezwa na watu wa kada hiyo hivyo kwa wale ambao hawatatimiza majukumu yao hasa ikiwemo wizi wa fedha hizo watoe taarifa.

Awali  Katibu wa Tume ya utumishi wa Walimu Nchini TSC,Paulina Nkwama  amesema  lengo la kikao hicho ni kujitahmini kuhusu majukumu ya Tume ambapo pia ameeleza malengo waliyoyatejeleza tangu kuanzishwa kwa Tume ya utumishi wa walimu  huku Mwenyekiti wa Tume hiyo,Profesa Willy Komba,amesema Mkutano kazi huo unalenga kujadiliana mada mbalimbali ikiwemo masuala ya ajira na maadili,rufaa uandaaji mashauri ya kinidhamu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »