WAZIRI NDALICHAKO AAGIZA WATENDAJI WA WIZARA NA TAASISI ZINAZOTEKELEZA MIRADI YA FEDHA ZA MPANGO WA MAENDELEO NA MAPAMBANO YA UVIKO 19 KUFIKIA OKTOBA 30,2021 MAANDALIZI YAWE YAMEKAMILIKA.

WAZIRI NDALICHAKO AAGIZA WATENDAJI WA WIZARA NA TAASISI  ZINAZOTEKELEZA MIRADI YA FEDHA  ZA MPANGO WA MAENDELEO  NA MAPAMBANO YA UVIKO 19  KUFIKIA OKTOBA 30,2021 MAANDALIZI YAWE YAMEKAMILIKA.

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Joyce Ndalichako amewaagiza watendaji wa Wizara na taasisi zitakazotekeleza miradi ya fedha za mpango wa maendeleo  kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uvico 19, hadi kufikia Octoba 30, 2021 wawe wamekamilisha mpango na maandalizi ya utelelezaji wa miradi hiyo. Hayo yamebainishwa leo jijini DODOMA na

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Joyce Ndalichako amewaagiza watendaji wa Wizara na taasisi zitakazotekeleza miradi ya fedha za mpango wa maendeleo  kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uvico 19, hadi kufikia Octoba 30, 2021 wawe wamekamilisha mpango na maandalizi ya utelelezaji wa miradi hiyo.

Hayo yamebainishwa leo jijini DODOMA na Prof. Ndalichamo  wakati akitoa mchanganuo wa fedha zitakazotekeleza miradi ya fedha hizo miradi ambayo ipo chini ya Wizara ya Elimu ambapo amebainisha kuwa kwa sekta ya Elimu imetengewa bilioni 368.9 ambapo Wizara ya Elimu imepata shilingi bilioni 64.9 kutekeleza miradi iliyochini ya Wizara hiyo.

Aidha,prof Ndalichako amesema hadi ifikapo Octoba 30, 2021 kila taasisi itakayotekeleza mradi huo iwe imekamilisha maandalizi na mipango ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango kazi utakao ainisha hatua mbalimbali za taratibu za manunuzi ya huduma na vifaa ambapo amesisitiza matokeo ya utekelezaji wa miradi yaendane na thamani ya fedha zilizotolewa huku akimuagiza katib mkuu wa wizara hiyo aandae mfumo wa uratibu, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi utakao wezesha kubaini changamoto zitakazo kuwa zikijitokeza na kuchukua hatua stahiki na kwa wakati.

Hata hivyo waziri huyo amebainisha kuwa fedha hizo zitakwenda kuimarisha ufundishaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo shilingi bilioni 1.47 zimetengwa, kuimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stedi ambapo kiasi cha shilingi bilioni 57.98 zimetengwa na kuimarisha mazingira ya utoaji elimu ya ualimu ambapo kiasi cha shilingi bilioni 5.44 zimetengwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »