HOSPITALI NCHINI KUZINGATIA MIKATABA YA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WATEJA

HOSPITALI NCHINI KUZINGATIA MIKATABA YA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WATEJA

Waziri wa afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amezitaka Hospital zote nchini kuzingatia Mikataba ya utolewaji wa Huduma bora kwa wateja. Dkt.Gwajima aliyasema hayo wakati wa mafunzo ya kwanza ya huduma Bora kwa wateja Yaliyofanyika Mkoani Morogoro chini ya uongozi wa Hospital ya Taifa ya Muhimbili. Alisema mikataba ya utoaji

Waziri wa afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amezitaka Hospital zote nchini kuzingatia Mikataba ya utolewaji wa Huduma bora kwa wateja.


Dkt.Gwajima aliyasema hayo wakati wa mafunzo ya kwanza ya huduma Bora kwa wateja Yaliyofanyika Mkoani Morogoro chini ya uongozi wa Hospital ya Taifa ya Muhimbili.


Alisema mikataba ya utoaji huduma  Bora kwa wateja ilianza kutekelezwa  tangu mwaka 2001 lakini baadhi ya watumishi wamekuwa hawazingatii na kujikuta wakiwasababishia usumbufu wagonjwa
“Utoaji wa Huduma bora kwa wateja Ni jambo muhimu Sana kwasabu mtu anapokuja hospitali haji kutalii anakuja kutetea na kulinda uhai wake, hivyo ni lazima apate huduma bora Tena kwa wakati Kama mikataba inavyoelekeza” alisema Dkt.Gwajima.


Aliwataka  watoa huduma ya afya nchini kuacha tabia ya kuwadharau na kuwanyanyasa wagonjwa wakidhani hawatambui haki zao.
Alifafanua kuwa kwa Sasa wananchi wengi wanajua haki zao katika kupatiwa Huduma bora za afya ndio maana wanapobaini mapungufu huchukua hatua za kutoa taatifa kwa mamlaka za juu
“Katika kipindi cha hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya wananchi wakiona wanafanyiwa ndivyo sivyo katika hospital zetu wanapiga picha na kusambaza mitandaoni kwasabu wanatambua haki yao ya kupata huduma bora Sasa niwatahadhatishe kwamba serikali haitamvumilia mtumishi atakayeendelea kukiuka mikataba ya utoaji Huduma bora kwa mteja” alisema Dkt. Gwajima.


Prof. Lawrance Muselu ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Mhimbili ambao ndio waandaji wa mafunzo hayo alisema lengo ni kuboresha utolewaji wa Huduma  katika sekta ya afya na kuongeza chachu ya utoaji Huduma bora kwa wateja.

 
Alibainisha mafunzo hayo yatafanyika kwa siku Tano ambapo pamoja na Mambo mengine pia yatasaidia Watumishi wote kuwa na dhana Mtambuka kwa kuzingatia taaluma na Maadili ya Kazi wawapo kazini ili kupunguza malalamiko kwa wananchi juu ya utolewaji wa Huduma za afya.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »