MAJALIWA: SERIKALI IMEENDELEA KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU NCHINI

MAJALIWA: SERIKALI IMEENDELEA KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU NCHINI

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu mbalimbali ya elimu kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu. Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watumishi wa umma na wakazi wa mkoa wa Lindi watumie

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu mbalimbali ya elimu kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu.

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watumishi wa umma na wakazi wa mkoa wa Lindi watumie kituo hicho kilichojengwa na Serikali kupitia fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kujiendeleza kitaaluma kwa manufaa yao pamoja na Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 26, 2021) baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Chuo Kikuu Huria mkoani Lindi pamoja na uzinduzi wa ugawaji wa madawati 1000 katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Mwanza, Tanga na Arusha akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani Lindi.

“Nimefarijika kuona mradi huu unaendelea vizuri na hizi ndio jitihada za Serikali na Mheshimiwa Rais Samia amesisitiza Watanzania wapate elimu karibu na makazi yao, hivyo ujenzi wa kituo hiki utawawezesha wahusika kupata taaluma katika mazingira bora.”

Waziri Mkuu amesema katika kuboresha miundombinu ya elimu ya awali Mheshimiwa Rais Samia ametoa shilingi bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa shule shikizi ili watoto wa Kitanzania katika maeneo mbalimbali nchini waweze kupata elimu karibu na makazi yao.

Naye, Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria Kituo cha Lindi, Neema Magambo amesema  ujenzi wa jengo hilo umegharimu shilingi milioni 378 ambao umehusisha ujenzi wa vyumba vya madarasa, vyumba vya ofisi, maktaba, vyoo na chumba cha kompyuta.

“Ikiwa ni chuo kikuu pekee katika mkoa wa Lindi, hivyo uwepo wa mradi huu utaongeza hamasa ya wadau wengi zaidi kusoma elimu ya juu hasa watumishi wa umma ambao kwetu sisi ni wadau wakubwa kwani moja ya lengo la uanzishwaji wa chuo hiki ni kuwawezesha kusoma wakiwa kazini ili kuongeza tija kwa Taifa.”

Amesema uwepo wa ofisi hiyo utaboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi wa Chuo Kikuu Huria kituo cha Lindi, ambapo awali walikuwa wanakaa katika ofisi moja kutokana na ufinyu wa nafasi pia chuo kitaondokana na gharama za kukodi ofisi pamoja na kumbi kwa ajili ya mitihani.

Akizungumza baada ya kuzindua kampeni ya ugawaji wa madawati Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza benki ya Exim kwa uamuzi wake wa kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati mashuleni na kuzishauri taasisi nyingine za kifedha kuiga mfano huo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »