SHULE 10 BORA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2021

SHULE 10 BORA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2021

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limeitaja shule ya msingi Graiyaki iliyopo mkoani Mara kuwa ndiyo shule iliyoibuka kinara kitaifa katika matokeo ya mtihani ya darasa la saba 2021. Akitangaza matokeo hayo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde aliitaja shule ya St Peter Claver iliyopo mkoani Kagera kushika nafasi ya pili.

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limeitaja shule ya msingi Graiyaki iliyopo mkoani Mara kuwa ndiyo shule iliyoibuka kinara kitaifa katika matokeo ya mtihani ya darasa la saba 2021.

Akitangaza matokeo hayo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde aliitaja shule ya St Peter Claver iliyopo mkoani Kagera kushika nafasi ya pili.

Rocken Hill iliyopo mkoani Shinyanga imeshika nafasi ya tatu huku Kemebos iliyopo mkoani Kagera ikishika nafasi ya nne, na nafasi ya tano imeenda katika shule ya Bishop Caeser iliyopo Kagera.

Kwema Modern iliyopo mkoani Shinyanga imeshika nafasi ya sita na St Magret iliyopo Arusha imeshika nafasi ya saba na shule ya Waja Springs ya Geita ikishika nafasi ya nane.

Kadama iliyopo mkoani Geita imeshika nafasi ya tisa na Chalinze Modern Islamic iliyopo Pwani imeshika nafasi ya kumi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »