Rais Dkt. Mwinyi ameweka mawe ya msingi katika ujenzi wa Hoteli mpya za kisasa.

Rais Dkt. Mwinyi ameweka mawe ya msingi katika ujenzi wa Hoteli mpya za kisasa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein AliMwinyi ameeleza haja kwa wawekezaji kuhakikisha miradi wanayoitekelezainawafaidisha wananchi wanaoishi karibu na miradi hiyo. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati akiweka mawe ya msingikatika ujenzi wa Hoteli mpya ya kisasa ya Riu Jambo iliyopo Nungwi pamoja na Hoteli yaEmerald Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi ameeleza haja kwa wawekezaji kuhakikisha miradi wanayoitekeleza
inawafaidisha wananchi wanaoishi karibu na miradi hiyo.


Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati akiweka mawe ya msingi
katika ujenzi wa Hoteli mpya ya kisasa ya Riu Jambo iliyopo Nungwi pamoja na Hoteli ya
Emerald Zanzibar Resort and SPA iliyopo Matemwe Mbuyuni Mkoa wa Kaskazini Unguja
ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kutimiza mwaka mmoja tokea aingie
madarakani hapo Novemba mwaka jana Novemba 2020.


Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi ambaye alifuatana na Mama Mariam Mwinyi
alisisitiza kwamba ni vyema miradi inayotekelzwa iwe inawafaidisha wananchi kwa
kuweza kupata ajira sambamba na kuweza kuuza bidhaa zao.


Alieleza kwamba ni vyema uongozi wa Mkoa na Wilaya ukaja kuweka utaratibu maalum
wa kuhakikisha bidhaa zao wanaziuza katika Hoteli hizo kwenye maeneo hayo badala ya
kuhangaika kutafuta masoko.


Aidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba ni vyema wawekezaji wa miradi hiyo wakaelewa
changamoto zinazoikabili jamii katika maeneo yenye miradi yao ili wakaweza kuwasaidia
hasa katika miradi ya elimu, afya, maji na mengineyo kwa kushirikiana na Serikali.


Rais Dk. Miwnyi alisema kuwa ni vyema vijana wakafaidika na kazi ama ajira katika
miradi hiyo zikiwemo Hoteli hizo za kisasa na kusisitiza kwamba kuna kila sababu ya
vijana katika maeneo hayo kuongeza ujuzi kwa kupata elimu inayokwenda na miradi
hiyo hasa ikizingatiwa kwmaba vyuo vya kutoa elemu hiyo vipo hapa hapa Zanzibar
kikiwemo Chuo cha Utalii Maruhubi.


Rai Dk. Mwinyi akiwa Matemwe Mbuyuni mara baada ya kuweka jiwe la msingi
akiwasalimia wananchi alieleza kwamba utalii ndio sekta muhimu inayoimarisha pato la
Taifa huku akisisitiza kwamba .


Rais Dk. Miwnyi aliwasisitiza vijana kUwa tayari kufanya kazi “Tuwe tayari kufanya
kazi…kwani kuna vijana wengi hawajawa tayari kufanya kazi, hivyo ni vyema wakawa
tayari na sisiSerikali iko tayari kufanya kazi kwa mashirikianio ya pamoja”,alisema Dk.
Mwinyi.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Mwinyi aliwapongeza wakandarasi wa ujenzi wa
Hotelihizokutokana na kasikubwa ya ujenzi wanayokwenda nayo ambayo inakwenda
sambamba na kasi ya Awamu ya Nane.

Nao wawekezaji wa Hoteli ya Riu Jambo ambapo ujenzi wake ulianza Januarimwaka huu
2021 waliwahakikishia wavuvi wa maeneo hayo kwamba mradi wa Hoteli yao
utakapokuwa tayari kufanya kazi samaki wote watakaovuliwa katika eneo hilo
watanunuliwa na hoteli yao ili kuhakikisha wavuvi hao wanapata soko la uhakika pamoja
na kuwajengea soko na miradi mengine ya jamii.


Kwa mujibu wa maelezo ya uongozi wa Hoteli hiyo, mradi huo unatarajiwa ujenzi wake
kumaliza mnamo Septemba mwakani 2022, na utaajiri wafanyakazi 400 huku hoteli
hiyo itakuwa na vyumba 468 ambapo ujenzi wake utagharibu zaidi ya Dola za
Kimarekani milioni 70.


Kwa upande wa Hoteli ya Emerald Zanzibar Resort and SPA ambayo ujenzi wake ulianza
Novemba mwaka jana 2020 unatarajiwa kumaliza mwakani 2022, mradi ambao kwa
akuanzia utakuwa na vyumba 250 na hadi kumaliza katika awamu zijazoitakwua na
vyumba 1000.

Kitengo cha Habari
Ikulu Zanzibar.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »