“Serikali itatumia sheria kuyalinda maeneo na kurudi kufanya biashara ni kosa”.Mkuu wa Mkoa Mhe.Makala

“Serikali itatumia sheria kuyalinda maeneo na kurudi kufanya biashara ni kosa”.Mkuu wa Mkoa Mhe.Makala

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amesema Katika *kuyalinda maeneo walipoondoka Machinga* Serikali itatumia *Sheria* kwa Wote *walioondoa Vibanda na kufanya Biashara Chini.*Akizungumza wakati wa *ziara ya kutembelea Maeneo mbalimbali walipohamia Machinga* kukagua changamoto ili Serikali izitatue, *RC Makalla* amewataka Wafanyabiashara waliokuwa *Kariakoo, Karume, Msimbazi* na Katika ya mji kufika *Machinga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amesema Katika *kuyalinda maeneo walipoondoka Machinga* Serikali itatumia *Sheria* kwa Wote *walioondoa Vibanda na kufanya Biashara Chini.*
Akizungumza wakati wa *ziara ya kutembelea Maeneo mbalimbali walipohamia Machinga* kukagua changamoto ili Serikali izitatue, *RC Makalla* amewataka Wafanyabiashara waliokuwa *Kariakoo, Karume, Msimbazi* na Katika ya mji kufika *Machinga Complex* ili wapatiwe nafasi ambapo mpaka Sasa *nafasi zilizosalia ni 2,100*.
*RC Makalla* pia amewaelekeza *Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi* kuanza rasmi *zoezi la Usafi* kwenye maeneo yote walipoondoka Machinga na kuhakikisha yanalindwa yasivamiwe upya.
Aidha *RC Makalla* amesema *Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zote* zitakazoonekana kwenye maeneo walipopelekwa ili Biashara zifanyike na *Wafanyabiashara wapate kipato.*
*Kwa mujibu wa sheria za miji na majiji zinaeleza kuwa kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa ni kosa kisheria ambapo adhabu kwa anaefanya kosa hilo ni kifungo Cha mwaka mmoja na faini ya Shilingi laki tatu.*

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »