WANAFUNZI 500 WASHINDWA KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA NNE KWA UTORO

WANAFUNZI 500 WASHINDWA KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA NNE KWA UTORO

 NA MWANDISHI WETU, MOROGORO MKUU wa wilaya ya Gairo Jabir Makame amesema zaidi ya wanafunzi 500 wa daraza la nne wilayani humo hawajafanya mtiani wa taifa kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro hali inayosababisha wilaya hiyo kuwa nyuma katika viwango vya ufauru DC Makame alibainisha hayo katika kikao cha baraz ala madiwani halmashauri ya gairo ambapo

 NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

MKUU wa wilaya ya Gairo Jabir Makame amesema zaidi ya wanafunzi 500 wa daraza la nne wilayani humo hawajafanya mtiani wa taifa kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro hali inayosababisha wilaya hiyo kuwa nyuma katika viwango vya ufauru

DC Makame alibainisha hayo katika kikao cha baraz ala madiwani halmashauri ya gairo ambapo alibainisha kuwa kukithiri kwa vitendo vya utoro ndio vinachangia kwa kiasi kikubwa kushisha ufaulu wa nanafunzi

“iko changamoto kubwa sana ya utoro kwenye wilaya yetu, kwa taarifa nilizonazo ni zaidi ya wanafunzi 500 hawakutokea kwenye mitihani ya darasa la nne kwasababu ya utoro, lakini pia kwa sasa hivi wakati mitihadi ya kidato cha pili inaendelea kesi za utoro bado zinaendelea” alisema Makame

Alisema hali ya kielimu kwa wilaya hiyo sio ya kuridhisha baada ya matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa wiki iliyopita yameonesha shule iliyoongoza kwa wilaya hiyo ni shule ya msingi Malowelo ina wastani wa 166.9 kati ya wastani wa 300

Alisema inashangaza kuona shule inayoongoza kwa wilaya ikiwa na wastani huo huku imeshika nafasi ya 200 kati ya shule 640 zilizopo mkoani morogoro na kuwataka wataaramu wa elimu kujitasmini katika uwajibikaji wa kukuza elimu wilayani humo

“mbali na changamoto ya utoro hata ufaulu nao ni tatizo haiwezekani shule inayoongoza kiwilaya ukija kwenye mkoa ikashika nafasi ya 200, kwa hiyo tunapata picha kwamba tunalitatizo kubwa katika idara ya elimu, kwenye eneo la udhibiti elimu, waratibu wa elimu, walimu wakuu na kwa wazazi na jamii kwa ujumla” alisema

Awali mwenyekiti wa halmashauri wialya ya Gairo hiyo Rechal Nyangasa alisema kuwa baraza hilo limewafuta kazi watumishi 33 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kugushi vyeti ya taaluma

Alisema kati yao watumishi 21 walitoa taarifa za uongo wakati wa kuajiriwa na wengine 10 wakifukuzwa kwa kushindwa kuwasilisha vyeti ya ufaulu wa kidato cha nne na wengine wawili wakifukuzwa kwa makosa ya utoro kazini.

“kwa mujibu wa kanuni na sharia watumishi hao wote 33 tumewafukuza kazi, lakini pia kwa mamlaka tulio pewa tumewabadirishia muundo watumishi 22 hawa ni wale ambao wamejiendeleza au wamebadiri kazi lakini pia huu mundo autahusika ma mishahara yao” alisema Nyangasa

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »