“Slovakia yakaribishwa kutengeneza magari yanayotumia haidrojeni”.Dkt. Budeba.

“Slovakia yakaribishwa kutengeneza magari yanayotumia haidrojeni”.Dkt. Budeba.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Musa Budebaameishawishi Slovakia kuwekeza Tanzania kwenye uchimbaji au ununuzi wa Madini yaViwandani yanayotumika katika kutengeneza vifaa vya teknolojia mbalimbali yakiwemomagari.Dkt. Budeba amemweleza Mkurugenzi wa Uchumi na Uwekezaji wa Kampuni ya Sarioinayomilikiwa na Serikali ya nchi hiyo Bw. Egon Zorad, kuhusu uwepo madini

Ujumbe wa Tanzania katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Uchumi na Uwekezaji wa Kampuni ya Sario ya Slovakia, Egon Zorad.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Musa Budeba
ameishawishi Slovakia kuwekeza Tanzania kwenye uchimbaji au ununuzi wa Madini ya
Viwandani yanayotumika katika kutengeneza vifaa vya teknolojia mbalimbali yakiwemo
magari.
Dkt. Budeba amemweleza Mkurugenzi wa Uchumi na Uwekezaji wa Kampuni ya Sario
inayomilikiwa na Serikali ya nchi hiyo Bw. Egon Zorad, kuhusu uwepo madini hayo ambayo
ni malighafi katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani.
‘’Tumeona Slovakia imepiga hatua katika masuala ya teknolojia ambapo wanatengeneza
magari yanayotumia haidrojeni na tumeona wametengeneza mifano ya ndege. Kwetu sisi
kama sekta ni fursa kuwavutia waje kuwekeza kwetu kwa ajili ya kupata malighafi ya
kutengeneza bidhaa zao kwa sababu vitu vyote tulivyoviona vinahitaji malighafi
zinazotokana na madini kama nickel, copper, rare earth elements, graphite na mengine
ambayo yote yapo kwetu,’’ amesema Dkt. Budeba.
Ametoa kauli hiyo wakati wa kikao na mwakilishi huyo aliyefika katika banda la Tanzania
baada ya wataalam wa Tanzania kutembelea banda la nchi hiyo katika Maonesho ya
Kimataifa ya Expo 2020 Dubai, ambapo walipata fursa ya kujionea teknolojia mbalimbali
zinazozalishwa na nchi ya Slovakia likiwemo gari linalotumia hydrojeni.
Kwa mujibu wa Zorad, gari hilo ambalo limetengenezwa kwa takriban miaka mitatu,
limetengenezwa na Vyuo Vikuu vya nchini humo kwa kushirikiana na Serikali na kampuni
binafsi. Wataalam wa watanzania baada ya kutembelea banda hilo walifahamishwa kuhusu
namna nchi hiyo inavyojaribu kukuza teknolojia zake na kuhamia katika mifumo mingine ya
kiteknolojia ikiwemo matumizi ya magari yanayotumia umeme.
Aidha, Dkt. Budeba amemuhakikishia mwakilishi huyo kuhusu upatikanaji wa rasilimali za
kutosha yakiwemo mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara yaliyopo nchini ikiwemo hali
ya usalama, na uwepo wa miundombinu ya kuwawezesha kufanya shughuli zao kikamilifu
huku pia, akieleza nia ya Tanzania kuunganishwa na wawekezaji wengine wakubwa kutoka
Slovakia.
Pia, mbali na kuchimba na kununua madini, Dkt. Budeba amemshawishi kuhusu kufikiria
namna Slovakia inavyoweza kuanzisha kampuni ya uundaji magari nchini Tanzania kutokana
uhakika wa upatikanaji wa rasilimali ambazo zitahitajika katika uundaji bidhaa hizo. Vilevile,
Dkt. Budeba amemuhakikishia kuwa, tayari Tanzania ina kanzidata yenye taarifa za kutosha
kuhusu uwepo wa madini hayo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya Sario, Bw. Zorad ameshukuru kukutana na
Wizara na kufahamishwa kuhusu uwepo wa rasilimali hizo na kutaka kupatiwa taarifa za
kutosha kuhusu masuala muhimu ya uwekezaji na biashara ya madini Tanzania ili pia
kampuni hiyo iweze kuiunganisha Tanzania na kampuni nyingine zilizoko Slovakia.

‘’Nataka sana Tanzania kuwa moja ya nchi tutakayoshirikiana nayo kwenye biashara na vyuo
vyetu. Tumeelezwa kuwa nchi yenu iko kwenye nafasi nzuri kibiashara katika masuala ya
madini. Slovakia tunaandaa mkutano wa wawekezaji na tunatarajia kualika angalau nchi
moja kutoka Afrika na haina shaka itakuwa Tanzania,’’ amesema Zorad.
Mbali na masuala yanayohusu madini, pia, mwakilishi huyo wa Kampuni ya Sario, ameelezea
nia ya Slovakia kutaka ushirikiano na Vyuo Vikuu vya Tanzania hususan kwenye masuala ya
utafiti.
Aidha, Dkt. Budeba na maafisa wengine wa Wizara ya Madini walifanya mkutano kwa njia
ya mtandao na mwekezaji kutoka China aliyetaka kuwekeza kwa kushirikiana Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO). Aidha Dkt. Budeba alimuunganisha mwekezaji huyo na Kaimu
Mkurugenzi wa STAMICO kwa hatua zaidi.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Banda la Tanzania kwenye Maonesha ya Expo 2020
Dubai, Bi. Getrude Ng’weshemi ameendelea kusisitiza ushiriki wa uhakika kama huu kwa
sekta nyingine ambazo zinatarajiwa kushiriki katika maonesho haya ili kuhakikisha Tanzania
inatumia vilivyo fursa zilizopo Dubai na kwingine duniani kupitia maonesho hayo.

Steven Nyamiti

Afisa Habari

Wizara ya Madini

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »