TIGO NA MILEMBE INSURANCE WAJA NA HUDUMA YA BIMA YA KIDIGITALI KWA VYOMBO VYA USAFIRI

TIGO NA MILEMBE INSURANCE WAJA NA HUDUMA YA BIMA YA KIDIGITALI KWA VYOMBO VYA USAFIRI

Leo Novemba 9, 2021 Kampuni inayoongeza kwa mapinduzi na utoaji wa huduma za kidigitali hapa Nchini Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya MILEMBE INSURANCE wamezindua Huduma mpya ya BIMA ya vyombo vya usafiri ijulikanayo kama TIGO MOTOR INSURANCE , huduma itakayowawezesha wateja wa Tigo Pesa kukatia vyombo vyao vya Usafiri Bima na

Leo Novemba 9, 2021 Kampuni inayoongeza kwa mapinduzi na utoaji wa huduma za kidigitali hapa Nchini Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya MILEMBE INSURANCE wamezindua Huduma mpya ya BIMA ya vyombo vya usafiri ijulikanayo kama TIGO MOTOR INSURANCE , huduma itakayowawezesha wateja wa Tigo Pesa kukatia vyombo vyao vya Usafiri Bima na kukamilisha taratibu zote muhimu Kidigitali kwa kutumia simu zao za mkononi popote pale watakapokua kupitia Tigo Pesa.

Bima hii itahusisha aina mbalimbali za magari kama vile Magari madogo ya kubeba mizigo, pikipiki, bajaji , Mabasi, Malori, Trekta , Mashine za Uchimbaji na mengineyo ambayo yamesajiliwa kwa matumizi ya Kibiashara na Binafsi.

Akizungumza katika Uzinduzi huo Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha amesema kuwa

“Takriban watu milioni 53.18 wanapata huduma za simu za mkononi nchini Tanzania lakini ni asilimia 13 tu ya watu wote wanapata huduma za Bima. Lengo letu ni kuendeleza huduma za bima ya kidijitali kote nchini, hasa kwa wale ambao wamepata ugumu wa kufikia huduma hizi kupitia njia zilizozoeleka .

Sekta ya Bima Tanzania inaendelea kuonyesha fursa nyingi za upanuzi na ukuaji, hii imejidhihirisha kupitia ongezeko la Taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utoaji wa Bima ambalo lina uwezekano wa kuongeza mahitaji ya bidhaa za bima kidigitali kupitia simu ya Mkononi, na sisi kama kampuni inayojali wateja wake ndio maana tukaamua kuja na TIGO MOTOR INSURANCE .”
“Ushirikiano wetu na bima ya Milembe (MILEMBE INSURANCE)
unalenga kuziba pengo la upatikanaji wa huduma za bima kwa kutoa suluhisho la kidijitali ambalo litapunguza gharama na kuongeza upatikanaji wa bidhaa za bima. Tunaamini kuwa zaidi ya wateja milioni 9 wa Tigo Pesa watatumia Huduma hii mpya ya bima, ambayo inapatikana kwa urahisi na gharama nafuu kabisa tena Kidigitali Alimalizia Bi. Pesha

Kwa upande wake Bwana Muganyizi Tibaijuka, Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Milembe Insurance amesema kuwa
“Bima ya Milembe wakiwa waanzilishi wa huduma ya Bima za Kidigitali nchini Tanzania maarufu kama BimaPap wana imani kuwa, kushirikiana na Tigo kunathibitisha kuwa ni hatua nyingine katika kuboresha ufanisi wa utendaji kazi na uhakikisho wa utoaji wa huduma bora kwa umma, hivyo basi kwa sasa wateja wa Tigo Pesa watapata unafuu wa kuvibimia vyombo vyao vya usafiri na kupewa Hati muhimu za Bima zao papo hapo kupitia simu zao, Aidha katika tukio la ajali ya gari ikiwa itawekewa bima kupitia Tigo Pesa , Mteja atatakiwa kuwasilisha taarifa ya madai kidigitali pasipo kulazimika kutembelea ofisi zetu na madai yake yataanza kushughulikiwa, hii inadhiirisha mustakabali mzuri kati ya Bima yetu na wateja wa Tigo Pesa Alimalizia Bwana Tibaijuka.

Kumbuka wateja wanaweza kusajili magari yao na kulipia BIMA kupitia MENU ya Tigo Pesa 15001#, chagua (7) huduma za kifedha, chagua (3) bima, chagua (2) bima ya magari, chagua (1) usajili wa gari, ingiza usajili wa gari. nambari, chagua (1) thibitisha na ujiandikishe, chagua (1) lipa, chagua matumizi ya gari, chagua (1) endelea kulipa, kisha weka pin ya Tigo Pesa ili kuthibitisha malipo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »