CMA CGM imeonesha nia ya kuwekeza kwenye usafirishaji wa madini Nchini.

CMA CGM imeonesha nia ya kuwekeza kwenye usafirishaji wa madini Nchini.

Tanzania imekutana na Kampuni ya CMA CGM inayojishughulisha na masuala ya usafirishajiwa mazigo yenye Makao Makuu yake Dubai ikiwakilishwa na Mkurugenzi wa Biashara wakampuni hiyo kwa upande wa Afrika Gulliaume Adam. Gulliaume ametaka kujua kuhusumaendeleo ya sekta ya madini na kueleza nia ya kampuni hiyo kusafirisha madini kutokaTanzania.Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Ukaguzi na

Wataalam kutoka Sekta ya Madini na Taasisi zake wakiwa katika kikao na
Mkurugenzi wa Biashara ya CMA CGM inayojishughulisha na masuala ya usafirishaji wa mizigo. Kampuni hiyo imeonesha nia ya kuwekeza katika Shughuli za usafirishaji wa madini kutoka Tanzania.

Tanzania imekutana na Kampuni ya CMA CGM inayojishughulisha na masuala ya usafirishaji
wa mazigo yenye Makao Makuu yake Dubai ikiwakilishwa na Mkurugenzi wa Biashara wa
kampuni hiyo kwa upande wa Afrika Gulliaume Adam. Gulliaume ametaka kujua kuhusu
maendeleo ya sekta ya madini na kueleza nia ya kampuni hiyo kusafirisha madini kutoka
Tanzania.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka
Tume ya Madini Bw. Venance Kasiki amemweleza mwakilishi huyo pia kuhusu uwepo wa
fursa nyingine mbali na ya kusafirisha madini ambazo kampuni hiyo inaweza kuzitumia
ikiwemo kuwekeza katika shughuli za uchimbaji na ununuzi wa madini.
‘’Sio tu biashara ya kusafirisha kuna fursa nyingi kwenye sekta ya madini nchini fikirieni pia
kuhusu kuchimba, kununua ama kusafirisha mizigo kwenye migodi. Msisite kuitumia Tume
ya Madini kupata taarifa zaidi kuhusu masuala haya. Serikali ipo karibu sana na wawekezaji
kwa hiyo msihofu kuhusu upotevu wa fedha wala udanganyifu,’’ amesema Kasiki.
Aidha, Kamishna Jenerali wa banda la Tanzania kwenye maonesho hayo Balozi Mohamed
Mtonga, baada ya kupata mrejesho wa Sekta ya Madini amezitaka sekta muhimu kwa ukuaji
wa uchumi na maendeleo ya taifa nchini kuchangamkia fursa kupitia maonesho hayo.
‘’Fursa hii ikipita imepita, tuitumie vizuri nafasi hii kuwaeleza tulivyonavyo nchini kwetu ili
waje kushirikiana nasi. Karibia dunia yote iko hapa na sisi tuna bahati kwamba hatuko
nyuma,’’ amesisitiza balozi Mtonga.
Hatua hiyo inafungua fursa ya uwekezaji katika Sekta ya Madini baina ya Tanzania na
wawekezaji kutoka nje ya Tanzania.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »