Watu Mil 4.7 wana magonjwa yasiyoambukiza.

Watu Mil 4.7 wana magonjwa yasiyoambukiza.

KATIKA kipindi cha mwaka 2016 hadi 2020 jumla ya watu milioni 4.7 wamebainika kuwa na magonjwa yasiyoambukiza baada ya kufanyiwa vipimo katika vituo na hospitali mbalimbali nchini. Akizungumza jana jijini Arusha juu ya maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo kitaifa yatafanyika Arusha kuanzia Novemba 6 hadi 13 mwaka huu,Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongela

May be an image of 2 people, people standing and outdoors
May be an image of 5 people, people standing and outdoors
May be an image of 2 people, people standing and text that says 'A NA KUDHIBITI MAGONJWA YASIYO 1/2021 MUDA: Saa 01:00 Asubuhi ja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha KAUL' Afy yaAfy Afy'
May be an image of 3 people and people standing

KATIKA kipindi cha mwaka 2016 hadi 2020 jumla ya watu milioni 4.7 wamebainika kuwa na magonjwa yasiyoambukiza baada ya kufanyiwa vipimo katika vituo na hospitali mbalimbali nchini.

Akizungumza jana jijini Arusha juu ya maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo kitaifa yatafanyika Arusha kuanzia Novemba 6 hadi 13 mwaka huu,Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongela alisema kutokana na takwimu hizo kuna haja ya kila mtu kuchukua hatua ya kukabiliana na magonjwa hayo.

“Idadi hii ya wagonjwa ni kubwa hivyo natoa wito kwa wananchi wa mkoa wangu kuzingatia aina ya vyakula wanavyokula na kufanya mazoezi ili kiepukana na magonjwa hayo ambayo dalili zake zinaanza taratibu na vigumu kugundua kwa haraka,”alisema.

Mongela alisema kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia 33 ya vifo vinavyotokea nchini vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza.

Alitaja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na pumu,shinikizo la damu,kisukari,ajali,saratani,kiharusi,shingo ya kizazi,tezi dume,ini,matiti,utumbo mpana na mengine.

Alima katika maadhimisho hayo Novemba 6 mwaka huu yatazinduliwa na Waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo Innocent Bashungwa.

Pia novemba 11 hadi 12 mwaka huu Waziri wa ElimuSayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako na Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu watashiriki maadhimisho hayo ambayo kilele Novemba 13 yatafungwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dk.Doroth Gwajima.

Aliwaasa wananchi kuepuka vyakula vya chumvi nyingi,sukari nyingi na kujitoleza kwa wingi kupima afya zao katika wiki ya maadhimisho hayo.

Meneja Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza Dk.Omari Ubuguyu aliwaasa wananchi kula vyakula visivyokobolewa,kula matunda badala ya Juisi,kula kiasi kuepuka unene na kula vyakula halisi ili kupunguza magonjwa hayo.

Pia alisema magonjwa hayo huanza taratibu na ya muda mrefu,lakini pia hayaambukizi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »